Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA), Richard Kayombo.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) yawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa
taarifa za Maafisa wanaofanya kazi kinyume na maadili.
Akiongea
na mwandishi wa habari hii leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa
Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA), Richard Kayombo amesema kuwa TRA
ina Idara Maalumu ijulikanayo kama Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA ambayo
inashughulika na kufuatilia maadili ya watumishi wa sekta hiyo nchi
nzima.
“Tunawaomba
wananchi kushirikiana na Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA kwa kuwapa
taarifa juu ya maafisa wa TRA wanaokwenda kinyume na Maadili ya Utumishi
wa Umma,”alisema Kayombo.
Mkurugenzi
Kayombo ameongeza kuwa wananchi wanaweza kutoa taarifa kwa kupiga simu
kwa namba 0689122515 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwa simu namba
0689122516 na kuwahakikishia kuwa taarifa zao zitakua zimefika sehemu
husika na zitafanyiwa kazi.
Aidha
Kayombo amependa kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa namba hizo ni za siri
na hakuna mwananchi atakayepata tatizo lolote kwa kutoa taarifa za
maafisa wasio na maadili.
TRA
kupitia Idara yake ya Mambo ya Ndani imepokea malalamiko mengi kutoka
kwa wananchi juu ya watumishi wa TRA wanaoenda kinyume na maadili,
wameyafanyia uchunguzi na baadhi ya watumishi wamefukuzwa na wengine
kupewa adhabu kali.
No comments:
Post a Comment