Usiku wa kuamkia January 08 2016 najua
kuna Watanzania ambao macho na masikio yao yalielekezwa Nigeria ambako
zilikuwa zinatolewa Tuzo za wakali wa soka Afrika.
Good news ni kwamba staa wa soka ambaye amekiongoza kikosi cha TP Mazembe kufanya vizuri michuano ya Afrika, Mtanzania Mbwana Samatta amefanikiwa kuibuka na ushindi wa Tuzo ya mchezaji bora wa soka Afrika mwaka 2015 kwa wachezaji wanaochezea Afrika.
Mbwana Samatta ndio jina liliotajwa zaidi kwenye vinywa vya watanzania wengi na Afrika kiujumla ndani ya masaa kadhaa yaliyopita baada ya mwanasoka huyo wa Kitanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika Anayecheza Ligi za Ndani ya Afrika.
Ushindi wa Samatta, ambaye ni mshindi wa namfungaji bora wa ligi ya mabingwa wa Afrika umetokana na kuwashinda wapinzani wake Zein Edin Farahat, Roger Assale, Robert Kidiaba, Moudather el Tahir,Mohammed Meftah, Kermit Erasmus, Felipe Ovono, Baghdad Bournedjah, na Abdeladim Khadrouf.
Utaratibu wa CAF – Shirikisho la soka katika upigaji kura wa kumchagua mshindi wa tuzo hii unatokana na kura zilizopigwa na makocha wa timu za taifa au wakurugenzi wa ufundi wa vyama vya soka vya nchi za kiafrika.
Kwa mwaka huu wachezaji wote hao waliotajwa hapo juu walipigiwa kura na matokeo ni kama yanavyoonekana kwenye mpangilio hapo chini.
Mbwana Samatta alipata jumla ya kura 127 na hivyo kuongoza, akifuatiwa kwa mbali na mchezaji mwenzie wa TP Mazembe Robert Kidiaba aliyepata kura 88 na aliyefunga Top 3 ni Baghdad Bournedjah. Kura zilipigwa na mataifa 45 ya nchi wanachama wa shirikisho la soka Afrika CAF.
No comments:
Post a Comment