Watu katika miji mbalimbali
walijitokeza kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2016 kwa njia mbalimbali. Huu
hapa ni mkusanyiko wa picha za hali ilivyokuwa.
Australia ilikuwa
moja ya nchi za kwanza kuingia mwaka 2016, fataki zinaonekana hapa juu
ya jumba la Opera House na daraja la Harbour Bridge.
Mjini Sydney
Nchini Misri, fataki zinaonekana zikilipuka karibu na Piramidi.
Mjini Cairo
Jijini Berlin, fataki zilitawala anga kama inavyoonekana hapa juu ya Lango la Brandenburg mjini Berlin.
Mjini Berlin
Mjini London, hivi ndivyo hali ilivyokuwa karibu na Big Ben. Maelfu ya watu walijitokeza kutazama fataki.
Mjini London
Mji wa Baghdad haukuachwa nyuma, na hapa fataki zinaonekana zikilipuka katika Bustani ya Zawra.
Mjini Baghdad
Mjini Singapore, mwaka mpya ulikaribishwa kwa fataki. Hapa ni Marina Bay.
Mjini Singapore
Mjini Kuala Lumpur, nchini Malaysia fataki zinaonekana zikilipuka karibu na jengo mashuhuri ya Petronas Towers.
Mjini Kuala Lumpur
Mjini Taipeni, Taiwan, fataki zinaonekana kwenye jumba refu la Taipei 101.
Mjini Taipei
Mjini Paris, watu walikusanyika Champs Elysees kutazama video ya Mwaka Mpya iliyoonyeshwa katika Arc de Triomphe.
Mjini Paris
Nchini India, mwanamume huyo alitumia nyanya, vitunguu na pilipili kuandika 2016.
Mjini Amristar, India
Mjini Auckland, New Zealand fataki zililipuliwa katika jumba la Auckland Sky Tower, mkesha wa Mwaka Mpya
New Zealand
Hapa, mwanamume anaonekana akitembea karibu na
mapambo yaliyoandika 2016 katika mji wa Kiev, nchini Ukraine. GDP ya
taifa hilo ilishuka asilimia 9 mwaka 2015.
Mjini Kiev
Mjini Brazil, baadhi waliamua kufika katika ufuko wa Copacabana mjini Rio de Janeiro kuukaribisha mwaka mpya.
Mjini Rio
Mjini Beijing watu wengi waikusanyika kwa hafla iliyokuwa Hekalu la Tai Miao karibu na Forbidden City mjini Beijing.
No comments:
Post a Comment