TTCL

EQUITY

Tuesday, January 26, 2016

Bunge kujadili hotuba ya Rais Magufuli siku 3

Mkutano wa Pili wa Bunge la Kumi na Moja unaanza leo tarehe 26 Januari, 2016 na kumalizika tarehe 5 Febuari Mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Bunge ni kwamba Kanuni ya 23 (1) (i) ya Kanuni za Bunge, toleo la Januari, 2016, Bunge litajadili Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyoitoa wakati wa ufunguzi rasmi wa Bunge jipya la Kumi na moja tarehe 20 Novemba, 2015 .
Mjadala kuhusu hotuba ya Mheshimiwa Rais unatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 26 hadi 28 Januari, 2016.
Hata hivyo ili kutoa nafasi kwa kila mbunge kuweza kuchangia bunge linatarajia kutengua kanuni na kuweka muda wa dakika 10 badala ya 15 za hapo awali kwa mbunge mmoja ili kutoa fursa kwa wabunge kuweza kujadili na kila mmoja apate nafasi,pia bunge liwe linaanza saa 10 jioni badala ya saa 11.

No comments:

Post a Comment