Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa, Mhe. Hussein Ali Mwinyi (Mb), aliyeteuliwa na kisha
kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri jeshi Mkuu
ameripoti ofisini na kuanza kazi rasmi.
Alipowasili ofisini kwake
alilakiwa na Naibu Katibu Mkuu, Mkuu wa Majeshi Mnadhimu Mkuu, Mkuu wa
Jeshi la Kujenga Taifa, wanajeshi na watumishi wa Umma wakiongozwa na
Katibu Mkuu wa Wizara, Bw. Job Masima waliojipanga nje ofisi.
Akiongea na Menejimenti, alisema
matarajio ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuongeza ufanisi, kupunguza
urasimu pamoja kupunguza matumizi ya matumizi ya serikali pasipo
kuathiri utendaji kazi.
Aidha, alisema Serikali ya Awamu
ya Tano imedhamiria kufanya kazi kwa kasi mpya ambapo Wizara yake nayo
inahitaji kuendana nayo.
Kwa awamu iliyopita Wizara
ilitekeleza majukumu yake ya msingi ya Ulinzi wa Mipaka na pamoja na
kusaidia Mamlaka za Kiraia pale ilipohitajika kufanya hivyo kwa
mafanikio. Kwa sasa kinachotakiwa ni kuendelea kufanya maboresho katika
utendaji kazi na kuleta ufanisi zaidi.
Licha ya kufanya kazi kwa ufanisi,
alikiri kuwa bado zipo changamoto chache zinazoikabili Wizara hii,
ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka iwezekanavyo.
Akizitaja changamoto hizo kuwa ni
pamoja na idadi ndogo ya Vijana wanojiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria,
ikilinganishwa na wanohitimu Kidato cha Sita, uboreshaji ya Mashirika
yaliyo chini ya Wizara pamoja na migogoro ya ardhi inayotkana na aidha
watu kuvamia maeneo ya Jeshi au kuchelewa kutoa fidia kwa wananchi
waliotwaliwa maeneo yao.
Waziri mwinyi ni miongoni mwa
mawaziri waliokuwa kwenye Baraza la Mawaziri katika Serikali ya Awamu ya
Nne. Na Awamu hii ya Tano ameteuliwa kwa mara nyingine kuingoza Wizara
hii.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ulinzi na JKT
No comments:
Post a Comment