Wajumbe
wa baraza la madiwani jimbo la ushetu Kahama wamelalamikia vitendo vya
Rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watumishi serikali likiwemo jeshi la
Polisi kitengo cha usalama barabarani huku wakiinyoshea vidole taasisi
ya kuzuia na kupambana na rushwa "TAKUKURU" kushindwa kuziba mianya ya
rushwa na badhi ya watumishi wake kushiriki kuendeleza vitendo hivyo.
Wakizungumza baada ya kuzinduliwa baraza jipya la madiwani jimboni
hapo baadhi ya madiwani waliopata nafasi ya kuchangia hoja wameitaka
TAKUKURU kuhakikisha inawakamata watendaji wote serikalini wanaoshiriki
kuendeleza vitendo vya Rushwa huku wengine wakihoji kuwa ni kwanini
watendaji wa vijiji na kata hawawezi kufanya kazi bila kudai Rushwa kwa
wananchi? Hali ambayo imekua ikirudisha nyuma maendeleo ya jamii.
Kwa upande mwingine madiwani hao wameitaka serikali kuanzisha
mpango mkakati wa kutoa elimu juu ya rushwa katika maeneo ya vijijini na
mijini kwakuwa wananchi wengi hawaelewi maana ya rushwa huku mwenyekiti
wa halmashauri ya ushetu Bw.Juma Kimisha akidai kuwa amejipanga
kudhibiti mianya ya rushwa hali itakayosaidia kuleta maendeleo ya haraka
kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment