Rais wa Zanzibar na Mweneyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein akikata utepe |
Rais
wa Zanzibar na Mweneyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein
amewahakikishia wazanzibari kuwa serikali imenunua meli mpya na
kuwakemea wale wanaopinga maendeleo ya seriklai kwa kutangaza meli hiyo
ni ya mtumba.
Dr.Shein ametoa kauli hiyo wakati akiongea na wananchi mara baada
ya kuizindua meli mpya ya kisasa ya mapinduzi 11 ambayo imenunuliwa na
serikali na iliwasili kutoka Korea wiki iliyopita,Dr.Shein amesema
serikali imechukua ya kununua meli hiyo baada ya kuona ajali za meli
zikipoteza maisha ya wananchi na ndio maana imeamua pia kutoruhusu
uletaji wa meli zilitumika hivyo amewataka wananchi wasibababishwe na
amneno ya wachache wasioitakia mema Zanzibar.
Amewahahkishia wananchi wa Zanzibar kuwa meli hiyo itataoa huduma
zaidi kwa kuwajali wananchi wake na itahakikisha nauli zake zinakuwa za
hali ya kuridhisha na hata serikali itafidia baadhi ya gharama huku
serikali ikendelea kumirisha uchumi wake kwa kujenga bandari mpya na
kubwa na kuimarisha miundombinu ya mawasilaino
Mapema katibu mkuu wa wizara ya mindombinu na mawasilaino Dr.
Juma Malik Akil amesema seriklai iemtumia dola za marekani kwa ajili
ya ujenzi wa meli hiyo na imekidhi viwango vya kimataifa na in uwezo
wa kuchukua abiria 1200,tani 250 za mizigo na magari zadi ya 80 huku
ikiwa na vifaa vyote vya kisasa vya uokozi na mawasilaino.
No comments:
Post a Comment