Chama
cha Demokrasia na maendeleo Chadema kimemtaka rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr,John Pombe Magufuli kuikubali ya rasimu ya
katiba ya Joseph Sinde Warioba yenye vipengele vya kuwapa maamuzi
wabunge kuyajadili kisha kuyapendekeza baadhi ya majina ya mawaziri
wateule ili kuepuka kuchagua mawaziri mizigo na wenye kashfa kwa nchi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika siku yake ya mwisho wa
mkutano wa kmapeni ya nafasi ya ubunge jimbo la Handeni mjini,naibu
katibu mkuu wa chadema taifa Mheshimiwa John Mnyika amesema hatua
inafuatia mheshimiwa rais kuchagua baadhi ya mawaziri wale wale
wanaotuhumiwa na kasfa ya escrow hatua inayowashawishi watakaporejea
bungeni kuanzisha tena mjadala huo.
Awali wakizungumza katika mkutano huo baadhi ya wabunge wa viti
maalum chadema wamewataka wananchi wa jimbo la handeni kukataa
kutawaliwa kifalme na badala yake wafanye mabadiliko ili kuwasaidia
akina mama waepukane na tatizo la ukosefu wa maji ambalo limesababisha
kukumbwa na magonjwa ya milipuko mara kwa mara ikiwemo kipindupindu.
Kufuatia hatua hiyo mgombea ubunge wa jimbo la handeni Bwana.Said
Lusewa amesema amebaini kuwa baadhi ya miradi ya maji imekuwa sio
endelevu kwa sababu mbali mbali za utendaji na badala yake atahakikisha
kuwa kipaumbele chake endapo atapewa ridhaa na wananchi ataanza na maji
kuanzia ngazi ya kitaifa na kimataifa ili wahisani waweze kuliona tatizo
hilo.
No comments:
Post a Comment