TTCL

EQUITY

Friday, December 4, 2015

Serikali yatakiwa kuhakikisha inaitazama sekta ya elimu nchini kwa jicho la kipekee.

Uwezo mdogo wa wahitimu katika ngazi mbalimbali za kielimu hapa nchini umetajwa kuwa unasababishwa na uwekezaji hafifu katika sekta ya elimu ambapo serikali imetakiwa kuhakikisha inaitazama sekta ya elimu kwa jicho la kipekee.
Kwa mujibu wa ripoti ya hali ya elimu kwa miaka 10 iliyopita nchini  inaonyesha mafanikio makubwa kwa sekta ya elimu huku ikitaja ongezeko la walimu, madarasa, wanafunzi, vitabu ikiwa ni pamoja na uwiano wa wasichana na wavulana wanaojiunga na kuhitimu elimu ya sekondari kuongezeka.
 
Licha ya uwepo wa ongezeko kubwa la msingi kutoka 14257 mwaka 2005 hadi 16538 mwaka 2015, shele za sekondari 1745 mwaka 2005 hadi 4753 mwaka 2015, huku pia vyuo vya ufundi vikiongezeka kutoka 184 mwaka 2005 hadi 744 mwaka 2015,kwa miaka 10 ripoti inasema uwezo wa wahitimu umeonekana kuwa hafifu zaidi.
 
Ili kuboresha sekta ya elimu nchini, ripoti imeitaja serikali ya rais Dkt John Magufuli kuhakikisha inaboresha miundombinu ya kufundishia katika shule za umma, kuboresha maslahi ya walimu, ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa sera za elimu,
 
Ripoti hiyo imeipongeza serikali ya awamu ya nne kwa kuimarisha bajeti ya elimu kutoka bilioni 669 mwaka 2005/6 hadi shilingi trion 3.4 mwaka 2014/5 ongezeko lililosaidia zaidi ya asilimia 98 ya watoto wenye umri wa kwenda shule kudahiliwa kuanza darasa la kwanza.

No comments:

Post a Comment