TTCL

EQUITY

Saturday, December 12, 2015

Nani yu huru?

Wakurupuka alfajiri, haraka wende kazini, Wajutia kuliacha shuka, waogopa kuchelewa. Ukifanyacho kimepangwa, mpangaji ni mwajiri, Muda ulohisi wako, ukweli si wako Mwajiri kaununua nira kakufungia Wajisifu na ajira?
 
Mwajiriwa akilinda kibarua chake
Uhuru ni nini na aliye huru ni nani?
Aliyehuru hufugwa na mwingine, ati?
Aliye huru yuna muda
Cha kufanya akipanga yeye, pa kwenda haamrishwi
Huenda atakako kwa hiari ya muda wake
Hupata mkate wake pasipo mauzo ya muda wake
U huru?
 
Mtumwa aongozwa na bwana wake
Hiari na aendako hanayo
Kazini ni lazima
Ujira huupata kwa kuuza uhuru wake
Hana mamlaka na muda alodhani wake
Muda wake kauuza kwa mwajiri
Nira kakabidhiwa
Mabega yote juu, meno yote nje
Ajisifu ana ajira!
Upendacho kukifanya, huthubutu kukifanya
Si wajua hakikupi muamala?
Usichopenda ndo' wakifanya kupata mkate wako
Kwa gharama ya muda wako mkate waupata
Muda huna shilingi wapata
Shilingi wapata kwa kumtumikia mwajiri
Na wadai u huru?

No comments:

Post a Comment