Moja ya matukio yaliyo uacha mwaka 2015 katika maajabu Mwezi usio wa kawaida waibua msisimko
Picha hii inaonyesha mwezi mkubwa wa kawaida na
mwezi mkubwa ukilingana na kupatwa kwa mwezi kama ilivyoshuhudiwa
Wiesbaden, Ujerumani Septemba 282015
Watu wengi pande
mbalimbali duniani wamekuwa wakitazama tukio la kawaida la kupatwa kwa
mwezi ambalo limetokea wakati mmoja na kuonekana kwa mwezi mkubwa kwa
Kiingereza "supermoon".
Mwezi huo mkubwa huonekana mwezi unapokuwa
karibu zaidi na njia ya mzunguko ya dunia, jambo ambalo huufanya
kuonekana mkubwa angani.
Mwezi mkubwa ulivyoshuhudiwa angani London
Kupatwa kamili kwa mwezi – ambako huufanya kuwa na
rangi nyekundu – kulionekana Amerika Kaskazini, Afrika Magharibi na
Ulaya Magharibi.
Mwezi mkubwa usio wa kawaida unavyotokea
Tukio hili lilitokea mara ya mwisho 1982 na mara nyingine litaonekana 2033.
No comments:
Post a Comment