Serikali imesema kuwa Licha ya juhudi za wadau wa
kimataifa na serikali, ugonjwa wa kipindupindu bado umeendelea kuuwa
watu wengi nchini Tanzania huku changamoto kubwa ikibainishwa kuwa watu
kutozingatia usafi wa mazingira na kanuni za Afya.
Mtaalamu wa afya ya jamii ya epodemiolojia Dk Azma Simba kutoka
wizara ya afya (Mwenye t-shirt Nyeusi) akiwaeleza jambo wataalam wa Afya
kutoka nje
Akizungumza
kwa njia ya Simu na East Africa radio mtaalamu wa afya ya jamii ya
epodemiolojia Dk Azma Simba kutoka wizara ya afya amesema kuwa licha ya
kwamba kwa baadhi ya mikoa mlipuko wa kipindupindu unadhibitiwa lakini
kwa ujumla ugonjwa unasambaa kwa kasi ambapo zaidi ya watu 12,000
wameripotiwa kuathirika na Ugonjwa huo.
Dkt. Simba amesema kuwa kile anachokiona kinakwamisha kutokomeza kwa kasi kipindipindu Tanzania ni kukosekana kwa ushirikiano toka kwa jamii katika kuitikia wimto wa utunzanji wa mazingira pamoja na kuzingatia kanuni za afya.
Takribani watu 200 wamefariki dunia kutokana na mlipuko wa kipindupindu nchini Tanzania ambao ulianza mnamo Agosti 15, 2015.

No comments:
Post a Comment