TTCL

EQUITY

Thursday, December 24, 2015

Rais Magufuli akamilisha uteuzi wa Mawaziri wanne wizara zilizokuwa zimebaki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la Mawaziri la kwanza katika awamu ya tano yautawala wake.
 hapa tuangazie kwanza baraza la awali ambapo kabla ya kumalizia wizara zilizobaki, aidha aliwateua hawa na kuwaamini kuwa ni watendaji wazuri..
 

BARAZA LA MAWAZIRI
Wizara ya Ofisi ya Ris, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora
Waziri – Geogre Simbachawene na Angella Kairuki
Naibu  – Sumeilam Jafo
Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
Waziri – January Makamba
Naibu – Luhaga Jerrson Mpina
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, Walemavu
Waziri – Jenista Muhagama
Naibu – Ktr. Possy Abdallah na Antony Muvande
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri – Mwigulu Nchemba
Naibu – William Ole Nasha
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri – (bado hajapatikana)
Naibu – Inj. Edwin Ngonyani
Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri – (bado hajapatikana)
Naibu – Ashantu Kizachi
Wizara ya Nishati na Madini
Waziri –  Prof. Sospeter Muhongo
Naibu – Medalled Karemaligo
Wizara ya Katiba na Sheria
Waziri – Harrison Mwakyembe
Waziri w Mambo ya Nje, Ushirikiano na Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Waziri – Dkt. Augustino Mahiga
Naibu – Dkt. Susan Kolimba
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri – Dkt. Hassan Mwinyi
Waziri ya Mambo ya Ndani
Waziri – Charles Kitwaga
Waziri wa Ardhi, Nyumba, Mendeleo na Makazi
Wsziri – William Lukuvi
Naibu – Angelina Mabula
Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri – (bado hajapatikana)
Naibu – Inj. Ramol Makani
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Waziri – Charles Mwijage
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi
Waziri – (bado hajapatikana)
Naibu – Inj. Stella Manyanya
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri –  Ummy Mwalim
Naibu –  Dkt. Hamis Kigwangala
Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo
Waziri – Nape Nnauye
Naibu – Anastazia Wambura
Wizara ya Maji ya Umwagiliaji
Waziri – Prof. Makame Mbarawa (amehamishiwa wizara)
Naibu – Inj. Isack Kamwela

Uteuzi uliobaki ni kama ifuatavyo;
1.Profesa Jumanne Maghembe -Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.
2.Dkt. Philip Mpango – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).
3.Mhandisi Gerson Lwenge – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
4.Dkt. Joyce Ndalichako – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.(Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)
5.Mheshimiwa Hamad Masauni – Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
6.Prof.Makame Mbarawa –Amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano.

Je, unamaoni gani kwa Mh. Rais, kuna wizara yoyote amepanga unadhani hakuitendea haki, naomba maoni yako...

No comments:

Post a Comment