TTCL

EQUITY

Friday, December 25, 2015

CHEGE; FACEBOOK IMENIBOA


Saidi Juma maarufu kwa jina la Chege Chigunda Mtoto wa Mama Saidi kutoka TMK alipokuwa akifanyiwa mahojiano ya mojakwamoja kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) kinachorushwa na chaneli ya EATV kila siku ya Ijumaa saa (04:05 - 06:00) usiku, ameongea hayo wakati akitambulisha video yake mpya ya SWEETY SWEETY.

Chege amefunguka na kusema wazi kuwa hayupotayari tena kuvumilia kuona jina lake likitumiwa vibaya na watu wasiojua utu wa mtu akiwalenga wanaotumia jina lake kujinufaisha katika mitandao ya kijamii ambapo alitaja kujiondoa Facebook kwakile aliche sema utakuta mtu anajiita Chege Chigunda alafu unamkuta ni muuza duka tu, siwezi poteza muda kwaajili ya watu kama hao kuwafuatilia. ni bora kujiondoa tu, staki tena Fb.

Aidha amemalizia kwa kuelezea mikakati yake ya mwaka ujao 2016 kuwa atahakikisha anapiga hatua kimuziki, "Nautazama muziki wangu Boda to Boda, na nakusudia kufikia malengo yangu ya kuuza muziki wangu nje ya east afrika na afrika kwa ujumla."

No comments:

Post a Comment