Mwanamuziki wa kizazi kipya Bob Junior |
Gazeti la Sani leo limeibuka na habari yenye kichwa cha habari, ‘Baada ya ndoa yake kuvunjika: Bob Junior aibuka kwa Vanessa Mdee.
Habari hiyo imeonesha kumkera msanii huyo aliyemshirikisa Vanessa kwenye wimbo wake ‘Bashasha’ na kuamua kuandika kwenye Facebook, “hichi ndicho walitaka kusema ,haya msha sema kingine kipi????’
Awali gazeti jingine la udaku liliandika habari kuwa Bob Junior huvaa nguo za ndani za kike ambazo kabla ya hapo zilidaiwa kuwa za mwanamke wa nje na kusababisha kuvunjika kwa ndoa yake.
No comments:
Post a Comment