Ni
wakati mwingine tunakutana tena kupitia safu hii ambayo kimsingi
tunakumbushana na kuelimishana juu ya mambo mbalimbali yanayogusa maisha
yetu ya kimapenzi. Naamini wewe msomaji wangu umzima bukheri wa afya na
uko tayari kabisa kupitishia macho kile ambacho nimekuandalia kwa siku
hii ya leo.
Mpenzi msomaji, hakuna kitu kinachouma katika uhusiano wa kimapenzi
kama kusalitiwa kiasi cha baada kufikia hatua ya kujiua ama kuwa vichaa
wanapokumbana na tatizo hilo.
Kwa wanaume, wengi wanapobaini kuwa wapenzi wao wanawasaliti wamekuwa
na kasumba ya kutunisha misuli na kuonesha umwamba kwa kuwatwanga
makonde au kuwafanyia mbaya wale waliowanasa nao kisha kuwaacha wapenzi
wao. Hili limebainika si jambo sahihi hasa linapotokea kwa watu wawili
waliotokea kupendana.
Kuna wengi ambao waliwafumania wake zao, wakawapiga na kuwajeruhi,
lakini wakajikuta hawakukomesha tatizo, zaidi ya kuwapa usugu wapenzi
wao wa kuendeleza wizi tena kwa dharau na kejeli huku wakibembelezana.
Kama nilivyosema awali, usaliti ni jambo linalouma kwa kiwango
kikubwa. Hakuna suala la kuazima mke katika maisha, watu huazimana
magari na pesa lakini mpenzi, hakuna jasiri wa namna hiyo! Huo ndiyo
ukweli wenyewe lakini, kupiga au kuacha unapobaini mpenzi wako
amekusaliti kunasaidia?
Jibu la kitaalumu ambalo naamini kuna wanaoweza kulikataa ni kwamba
hakusaidii. Hakusaidii kwa sababu, ukimpiga hiyo ni adhabu inayoishia
hapo hapo, kesho wanakutana, wanakusaliti tena kupozana machungu.
Ukimwacha utakutana nao mitaani wakiwa wameshikana mikono kwa uhuru
na raha zao, wewe utaumia sana moyoni mwako. Ukiwaua na wewe utauawa,
huku wanadamu wenzako wakikucheka kwa uzembe wa kufikiri.
Jamani usaliti upo si tunawaona wake na wapenzi wa watu wanaingizana gesti kila siku?
Hivyo basi, kama hujamfuma mpenzi wako leo kuna siku utakutana na meseji kali za kimahaba zikitoka ama kwenda kwa mwanaume mwingine. Utafanyaje baada ya kubaini hivyo?
Hivyo basi, kama hujamfuma mpenzi wako leo kuna siku utakutana na meseji kali za kimahaba zikitoka ama kwenda kwa mwanaume mwingine. Utafanyaje baada ya kubaini hivyo?
Maana kama ni tukio basi utakuwa umelishuhudia laivu bila chenga.
Wiki hii nataka kutumia safu hii kuwaelimisha wanaume wenzangu adhabu
sahihi ya kumpa mpenzi wako pale utakapomfumania ama utakapobaini
anakusaliti kwa namna moja ama nyingine.
Wanaume katika suala hili wanatakiwa kuweka kando mambo ya mabavu.
Ndiyo maana leo nasema hivi, ukimfumania mpenzi au mkeo, fuata hatua
hizi nne katika kukabiliana na tatizo hilo bila madhara. Kwanza piga
moyo konde, pili ondoka eneo hilo tena kwa kukimbia. Ukifika nyumbani,
endelea kunywa maji ili kupoza presha.
Akirudi mpenzi wako jitahidi kumkaribisha kwa mahaba na usimuulize ulichoona.
Nakwambia ukifanya hivyo mpenzi wako ataumia sana na hataendelea kukusaliti kwa kuwa atakuwa anawaza ni hatua gani unafikiria kumchukulia.
Nakwambia ukifanya hivyo mpenzi wako ataumia sana na hataendelea kukusaliti kwa kuwa atakuwa anawaza ni hatua gani unafikiria kumchukulia.
Na kwa yule uliyemshika naye, vivyo hivyo usizozane naye, mwache!
Utashangaa anahama eneo maana atakuwa anafikiri unamwandalia kombora kumbe umeamua kujituliza tu!
Utashangaa anahama eneo maana atakuwa anafikiri unamwandalia kombora kumbe umeamua kujituliza tu!
Wanasaikolojia wamethibitisa adhabu hii kuwa ina uchungu kuliko
kupiga au kukemea licha ya kwamba inahitaji ujasiri wa hali ya juu.
No comments:
Post a Comment