TTCL

EQUITY

Wednesday, November 25, 2015

Timu wenyeji huchangia kuharibu viwanja - TPLB

Bodi ya ligi nchini TPLB imesema inaendelea na maandalizi ya ya ligi hususani kwa upande wa viwanja ambavyo vingi vimeharibika na wameshatoa maelekezo ya jinsi ya kutunza viwanja hapa nchini.
Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface Wambura amesema, changamoto zilizojitokeza baada ya ligi kusimama kubwa ni viwanja ambavyo vimeharibika kutokana na utunzaji kuwa mdogo.
Wambura amesema, kabla ya kuanza kwa ligi walikagua viwanja vyote na wakavipitisha lakini matumizi ya viwanja hivyo ikiwemo matumizi kwa timu wenyeji kufanyia mazoezi pamoja na shughuli nyingine nje ya soka yamechangia kuharibika kwa viwanja hivyo.
Wambura amesema, wamekwisha waandikia wahusika ili kuwasaidia jinsi ya kulinda viwanja hivyo ili viweze kutumika muda mrefu kwa kazi husika.

No comments:

Post a Comment