Kikosi
cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinachodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro Premieum Lager kimewasili salama katika mji wa Blantyre
nchini Malawi jioni ya jana tayari kwa mchezo wa marudiano siku dhidi ya
wenyji siku ya jumapili.
Stars
inayonolewa na makocha wazawa Charles Boniface Mkwasa na Hemedi Morocco
iliondoka jana kwa usafiri wa shirika la ndege la Fastjet na kuwasili
jiji la Lilongwe saa 4 asubuhi kabla ya kuanza safari ya bus kuelekea
Blantayre iliyochukua takribani masaa 3.
Wachezaji
wote wapo katika hali nzuri kuelekea katika mchezo wa marudiano dhidi
ya Malawi siku ya Jumapili ambapo Stars itashuka dimbani kusaka matokeo
mazuri yatakayoiwezesha kufuzu kwa hatua ya pili, katika mchezo wa awali
uliochezwa jijini Dar es salaam, Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2 -
0.
Stars
inatarajiwa kufanya mazoezi kesho jioni katika uwanja wa Kamuzu Banda
uliopo Blantyre, uwanja ambao utatumika kwa mchezo wa siku ya Jumapili.
Kuelekea
mchezo huo wa marudiano, Kocha wa Stars Charles Mwasa amesema vijana
wake wote wapo katika hali nzuri kiafya, kifikra na morali ni ya hali ya
juu kuelekea kwenye mchezo huo.
Katika
hatua nyingine mabus mawili yenye washabiki wa Stars Supporter yako
njiani kuelekea nchini Malawi kwa ajili ya kuipa sapoti timu ya Taifa
(Taifa Stars) katika mchezo huo wa Jumapili.(P.T)
No comments:
Post a Comment