ARUSHA MJINI CHADEMA MADIWANI 24 NA CCM 1.ROMBO CHADEMA 27 NA CCM 1.TUNDUMA CHADEMA IMECHUKUWA MADIWANI WOTE 19,NA KWA NASSARY ARUMERU MASHARIKI NI CHADEM AVITI VYOTE 26 NA MOSHI VIJIJINI CHADEMA 15 NA CCM 1
Pia tunahakikisha taarifa za Ushindi wa Kingewndu,Bulaya na Wengneo akiwemo Zitto Kabwe NA HUKO IRINGA MJII HADI IMETANGAZWA KATA 13 Kati YA 18 NA ZOTE CHADEMA INAONGOZA ..RASIMI:Ester Matiko (Chadema) AMETANGAZWA KUWA MSHINDI JIMBO LA TARIME MJINI.
MATOKEO ARUMERU;
Kata za Shambarai Burka, Mbuguni, Kikwe, Nkoaranga, Usa River, Poli, Songoro, Seela Sing'isi, Nkoanekoli, Ambureni, Malula, Maji ya Chai, Imbaseni, Kikatiti, Ngabobo, Uwiro, Nkoanrua, - madiwani wa CHADEMA WAMETANGAZWA.
.,pia kupitia akaunti yeke nyingine Nasari kaandika haya;-'' Joshua Nassari ·
Jimbo lilikuwa na vituo 437, nimeshinda vituo 436. Nimeshindwa kimoja kwa kura 2.
LANDSLIDE VICTORY IN ARUMERU MASHARIKI. Leading in 436 polling stations out of 437.
Ukurasa wa facebook wa Mh.Lwakatare yeye alikuwa anagombea kwenye jimbo la Bukoba Mjini akichuana na mh.Hamis Kagasheki yeye kayaandika haya;-Wilfred Lwakatare
Na sasa umefika wakati wa mabadiliko kwa WATANZANIA.
Mmeyakubali na TUNAAHIDI kuto waangusha watanzania.
SERIKALI YA WANANCHI WOTE IMEKUJA SASA.
Ahsante wanabukoba kwa kunituma Mimi na madiwani WA UKAWA 10/14. TUTAWATUMIKIA!
mh.Mch.Piter Msigwa yeye alikuwa anatete Jimbo lake la Iringa Mjini mwenye kayaandika haya kupitia facebook yake;-Peter Msigwa
Iringa mjini MPAKA sasa tuna kata zilizotangazwa rasmi 13 Kati YA 18 , Maana yake tutaunda halmashauri, Asante iringa!
Katika Jimbo la Bunda Mjini ambalo lilikuwa linaongozwa na mh.Steven Wasira mgombea wa CHADEMA aliekuwa CCM mh.Esta Bulaya kayaandika haya kupitia akaunti yake ya facebook;-Ester Bulaya
Hakuna kisichowezekana chini ya jua, asante wanabunda,kwakuniamini, hatimaye ameng'oka.mungu wangu asante kwa kunisiimamia. Nimeshinda nasubiri kutangaza rasmi.
,,,,,
Mbunge aliyemaliza muda wake lakini anagombea tena Joseph Mbilinyi
Matokeo ya Ubunge Mbeya Mjini yatatangazwa leo jioni saa kumi na moja lakini matokeo ya udiwani Mbeya Mjini Chama Cha Chadema kimepata kata 26 huku CCM imepata kata 8 na kata 1 imeahirishwa kufanyika uchaguzi kutokana na mgombea kufariki dunia
Jimbo la Mbinga Vijijini
Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Mbinga Vijijini Martin Msuha ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
Jimbo la Monduli
Ubunge: Julius Kalanga (Chadema) 35,024 na Namelock Sokoine (CCM) 25,925.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo la Monduli, NduguJulius Kalanga ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
Jimbo la Siha
Ubunge: Dk Godwin Mollel (Chadema) 22,746 na Aggrey Mwanry (CCM) 18,584.
Msimamizi wa Uchaguzi, Rashid Kitambulio amemtangaza Dk Mollel kuwa mshindi wa jimbo hilo ambalo mbunge wake alikuwa ni Aggrey Mwanry (CCM).
Jimbo la Tunduma
Ubunge: Mwakajoka Frank (Chadema) 32,442, Frank Sichalwe (CCM) 17,220, James Mwakalonge(TLP) 85, Reddy Makuba (ACT Wazalendo) , 319.
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Tunduma, Halima Mpita ametangaza matokeo hayo.
Jimbo Buyungu
Ubunge: Bilago Samson Chadema), 23,041 na Christopher Chiza(CCM) 22,934
Mgombea ubunge wa Chadema Bilago Samson amefanikiwa kunyakua Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kwa kura 23041.
Jimbo hilo lilikuwa chini ya CCM kupitia Waziri Christopher Chiza aliyepata kura 22934.
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Kakonko, Jaina Msangi ametangaza matokeo hayo
Jimbo la Tarime Mjini
Ubunge: Ester Matiko(Chadema) 20,017, Michael Kembaki(CCM), 14, 025, Deogratias Meck(ACT-Wazalendo) 356.
Msimamizi mkuu wa Uchaguzi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Juma Mwajombe amemtangaza Matiko kuwa mshindi katika Jimbo hilo
Jimbo la Lindi Mjini
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Lindi Mjini, Ndugu Hassan Suleiman Kaunje ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
Jimbo la Tandaimba
Mgombea wa CUF/UKAWA Jimbo la Tandaimba Mtwara Ahmed Katani Katani ameibuka mshindi na kutangazwa rasmi kuwa mshindi katika jimbo hilo
No comments:
Post a Comment