Kikosi cha Olympic Stars cha nchini Burundi kilichochuana vikali na Stend United ya Shinyanga Tanzania.
Kampuni
ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Acacia iliingia mkataba wa miaka
miwili na timu ya Stend United ya Mkoani Shinyanga kwa ajili ya
kushiriki ligi kuu ya Vodacom ambayo inategemewa kuanza tutimua vumbi
katikati ya mwezi huu. Stand United ni moja kati ya timu bora kabisa
katika kanda ya ziwa ambayo imeshiriki katika ligi kuu msimu uliopita
2014/2015 na kumaliza ikiwa nafasi ya tisa.
Udhamini
wa ACACIA katika misimu hii miwili ya ligi kuu itasaidia katika
kuifanya timu ya Stand United iweze kufanya vizuri katika michezo yake,
pamoja na kusaidia katika kuboresha programu mbalimbali za timu na
kuendeleza vipaji pamoja na masuala ya Utawala.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Makamu wa rais wa Acacia aneshughulikia masuala ya kampuni, Deo Mwanyika, amesema “Kwa
takriban mwaka mmoja, tumekua tukifanya kazi pamoja na Stand United.
Kwa muda huo tulianzisha mchakato wa kutambua namna nzuri ya kuboresha
ushirikiano wetu ili kunufaisha watu wa Shinyanga na Kanda ya Ziwa kwa
ujumla.
Bwana
Deo amesema Msimu uliopita uliwapatia fursa nzuri ya kushuhudia uwezo
wa timu hiyo hasa ukizingatia ilikua mara yao ya kwanza kushiriki ligi
kuu, “Baada ya tathmini ya kina, tunadhani huu ni muda muafaka wa sisi
kusaini makubaliano au mkataba wa kuidhamini na kufanya kazi pamoja ya
kuikuza timu hii ya nyumbani maarufu kama “Chama la wana”.
Hivyo,
Leo, Acacia tunasaini mkataba na timu ya Stand United kwa udhamini wa
misimu miwili ya ligi kuu, wenye thamani ya Shilingi bilioni moja.
Udhamini huu unajuamuisha shughuli za uendeshaji wa timu, kuboresha
uongozi na kukuza vipaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Stand United Amani Vincent,
amesema udhamini huo wa miaka miwili utakuwa chachu kwa timu yake
kufanya vizuri katika ligi kuu, “Msimu uliopita tulimaliza tukiwa nafasi
ya nane na kipindi hicho hatukuwa na fedha ya kutosha kuendesha timu,
lakini kwa udhamini tulioupata kutoka kwa ndugu zetu wa Acacia vijana
wetu safari hii watafanya vizuri zaidi.
Kampuni
ya Acacia ni kampuni inayoongoza kwa shughuli za uchimbaji wa madini
hapa Tanzania huku ikiwa na Migodi mitatu katika kanda ya ziwa, kupitia
mradi wa “Acacia Maendeleo Fund” ambao ndio pia umetoa udhamini wa timu
ya Stend umekuwa pia ukitekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa
Jamii hapa nchi huku kampuni hiyo ikieleza kuwa dhamira yake ni
kuendelea kufanya kazi na Jamii zinazowazunguka katika kuwaletea
Maendeleo wenyeji.
|
No comments:
Post a Comment