Mapema leo Mhe. Harrison Mwakyembe amekanusha vikali tuhuma zilizokuwa zinaelekezwa kwake kwamba ameapa kudili na Edward Lowassa katika sakata la Richmond.
Amesema amekwisha kamilisha hatua za awali za kutoa taarifa katika mamlaka zinazohusika ikiwemo Polisi Makao Makuu Kitengo cha Cyber Crime, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili waweze kubaini mtandao huo ambao ulianza harakati zake tangu Lowassa atangaze nia.
"Sio uungwana kuchezea majina ya watu wanaokosa ujasiri wa kuelezea hisia zao hadi watumie majina ya watu wengine, mtandao huo nauona kuwa ni hatari"
Amesema huenda kwa sababu ya joto la uchaguzi suala hilo nipo katika msukumo wa kisiasa huku akitaka hatua kali ziweze kuchukuliwa.
Ameapa kupambana na kundi hilo "Nimedhamiria kukomesha tabia hii, nimekwenda Polisi Kitengo cha Cyber Crime (Mkosa ya Jinai ya Mtandao) na TCRA, kulalamikia mchezo huu hatari wa kihuni na tayari vyombo hivi vimeanzisha uchunguzi huu mkali, ili kubaini wahusika wote wanaoandaa hizo taarifa na kuzituma kwenye sehemu mbalimbli na wanaozituma sehemu nyingine hizo taarifa, lakini lazima tupeleke ujumbe ulio wazi kwa sababu nchi yetu inaendeshwa kwa misingi ya sheria"
Hata hivyo, amesema kundi hilo lilianza polepole, na Tanzania Daima amelitaja kuwa lilikuwa mbele sana kwa kuandika habari kuwa "Mwakyembe na Sitta Kujibu Mapigo" na waliandika bila kunihoji.
Amesema baada ya kupata taarifa hizo aliingia kwenye Mtandao Maarufu nchini wa JamiiForums.com unaoendesha mijadala kwa jamii.
Taarifa hizo aliziona kwenye blogs nyingi akakuta habari hizo lakini cha kushangaza ni pale alipoona taarifa hiyo Mwanahalisi Online kwamba amesema atapambana kufa na kupona ili Lowassa asiingie Ikulu.
Sasa hawa Mwanahalisi sijawahi kuongea nao ikifuatiwa na taarifa nyingine kuwa nimesema Lowassa hana sifa.
No comments:
Post a Comment