Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akiingia jengo la Utawala la Mkoa wa Arusha ili kukutana na Uongozi wa Mkoa huo kupata taarifa ya Mkoa inayohusu migogoro ya ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akipokelewa na Uongozi wa Mkoa wa Arusha alipowasili kufanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero za ardhi zilizoko katika Halmashauri mbalimbali za Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda akiwakemea watendaji wa ardhi Mkoani Arusha kutokana na umangimeza wao unaowafanya kushindwa kutatua kero za ardhi na kusababisha migogoro mingi ya ardhi mkoani humo. Alisema maafisa ardhi na mipango miji wanalalamikiwa sana na wananchi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akielezea mambo mbalimbali yahusuyo ardhi na mipangomiji kwawatendaji wa Mkoa wa Arusha(hawapo pichani) alipozungumza nao kwenye hoteli ya Naura Springs Arusha jana. Waziri Lukuvi amesisitiza nidhamu ya kazi na kufuata sheria katika kuhudumia wananchi masuala yahusuyo ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akikabidhiwa makabrasha yenye kero mbalimbali za ardhi zilizowasilishwa kwake kwa ufasaha mkubwa na Mkoa wa Arusha kupitia Mpima Ardhi wa Mkoa wa Arusha Bw. Hamdoun Mansoor.
Mbunge wa Arusha Mhe. Godbless Lema naye alikuwepo hoteli ya Naura Spring kuzungumzia migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi kwenye mkutano ulioandaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nassari naye alikuwepo hoteli ya Naura Spring kuzungumzia migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi kwenye mkutano ulioandaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi.
Mbunge wa Arumeru Magharibi Mhe. Goodluck Ole Medeye naye alikuwepo hoteli ya Naura Spring kuzungumzia migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi kwenye mkutano ulioandaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuv
Baadhi ya watendaji na viongozi mbalimbali wa Halamashauri za Mkoa wa Arusha wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi alipowakutanisha katika Hoteli ya Naura Springs kuzungumzia kero na migogoro ya ardhi katika mkoa huo kwa nia ya kuipatia ufumbuzi wa haraka.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akionyeshwa na Mpima Ardhi wa Mkoa wa Arusha Bw. Hamdoun Mansoor ramani yenye mipaka katika maeneo yanayobishaniwa kwenye mgogoro wa ardhi kati ya Wilaya za Arumeru, Monduli na Longido.Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akiongea na waandishi wa habari katika eneo lenye mgogoro wa ardhi lililoko mpaka wa Longido, Monduli na Arumeru eneo la Oldonyosambu Arusha. Waziri ameahidi kukutana na wanasiasa wa Mkoa wa Arusha ili kumaliza mgogoro huo.
No comments:
Post a Comment