TTCL

EQUITY

Monday, March 16, 2015

Ukeketaji Uingereza:Polisi walaumiwa

Maafisa wa polisi wamelaumiwa nchini Uingereza kwa kutowashtaki watu wanaotekeleza kitendo hicho.

Wabunge wa Uingereza wamewalaumu wakuu wa polisi na afya, kwa kushindwa kuwashtaki na kukamilisha kesi dhidi ya watu wanaohusika na kukeketa wasichana.
Wabunge wa kamati ya mambo ya ndani ya nchini humo, wamesema hakuna kesi hata moja iliyofanikiwa kupata hatia dhidi ya mshtakiwa, ingawa kuna maelfu ya visa kama hivyo.
Walisema kuna maafisa ambao hawafanyi kazi yao sawa-sawa.
Kamati hiyo imesema madaktari wanafaa kuhimizwa kuripoti visa kama hivyo kwa polisi, na washtakiwe iwapo hawafuati maelekezo.

No comments:

Post a Comment