MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete jana alianza ziara kwenye Jimbo hilo ambapo ametembelea shughuli mbalimbali pamoja na kujua changamoto zilizopo kwenye Jimbo lake.
Ridhiwani alitembelea kata ya Pera na kuzungumza na wakazi wa vitongoji mbalimbali ambavyo vinaunda kata hiyo ambapo leo ametembelea kata ya Kibindu nako alipata fursa ya kuzungumza na wakazi wa vitongoji vilivyopo kwenye kata hiyo.
Mbunge huyo atakuwa na ziara ya wiki moja kutembelea kata mbalimbali za Jimbo hilo na kujionea shughuli za maendeleo kama vile ujenzi wa shule za msingi na sekondari, barabara, zahanati na kufanya mikutano ya hadhara ya wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete Akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kitongoji cha Malivundo wakati wa ziara yake ya kutembelea shughuli za maendeleo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiongea na moja ya wanafunzi wa shule ya Msingi Malivundo wakati wa zaiara yake kutembelea shughuli za maendeleo kwenye Jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiweka mchanga kwenye mashine ya kufyatulia matofali alipotembelea ujenzi wa shule ya Msingi wakati wa ziara yake ya kutembelea shughuli za maendeleo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wananchi wa Jimbo lake wakati ziara zake.
Baadhi ya wakazi wa Kitongoji cha Malivundo wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete hayupo pichani alipotembelea Kitongoji hicho kwenye ziara yake ya kutembelea shughuli mbalimbali za maendeleo.
No comments:
Post a Comment