TTCL

EQUITY

Monday, March 2, 2015

MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA MSIBANI KWA KAPTENI JOHN KOMBA

 Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Kapteni John Komba aliyefariki jioni ya tarehe 28 februari 2015 jijini Dar es salaam,kushoto ni mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete.

 Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mke wa marehemu Kapteni John Komba nyumbani kwake Mbezi Tangi Bovu

 Wasanii wa TOT wakilia kwa uchungu msibani

 Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Fredrick Sumaye akisalimiana na wasanii wa TOT wakati akiwasili msibani.

 Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Fredrick Sumaye akisaini kitabu cha maombolezo kwenye msiba wa Kapteni John Komba.

 Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Fredrick Sumaye akimpa pole mke wa marehemu Kapteni John Komba.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa  Nape Nnauye akisaini kitabu cha maombelezo kwenye msiba wa Kapteni John Komba.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anna Makinda akisaini kitabu cha maombelezo ya msiba wa Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba.


Marehemu Keptain John Komba enzi za uhai wake


Mbunge na Mwimbaji maaarufu wa nyimbo za Siasa nchini Tanzania, Keptain John Komba amefariki dunia siku ya jumamosi jioni.

Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama tawala cha Tanzania chama cha Mapinduzi Nape Nnauye Mbunge huyo ambaye alikuwa maarufu kwa utunzi na uimbaji wa nyimbo za kampeni za chama hicho kifo cha chake kimetokea siku ya jumamosi majira ya jioni.

Marehemu Kaptain Komba alizaliwa Marchi 18 mwaka 1945 alipata elimu ya msingi huko nchini Tanzania katika shule ya Lituhi baadae elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Songea iliyopo kusini mwa Tanzania kuanzia 1971 hadi mwaka 1974.

Mwaka 1975 hadi mwaka 1976 Marehemu John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo Kleruu Iringa, Kusini Magharibi mwa Tanzania ambapo alihitimu cheti cha ualimu.

Marehemu John Komba ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli kaskazini mwa Tanzania mwaka 1978 hadi mwaka 1978.

Keptain John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka chuo Kikuu cha Washngton International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.

No comments:

Post a Comment