TTCL

EQUITY

Monday, March 2, 2015

MWIZI WA GAUNI LA LUPITA NYONG’O ALIRUDISHA BAADA YA KUGUNDUA NI FEKI NA HALINA THAMANI YA $150,000

Mwizi aliyeiba gauni la muigizaji Lupita Nyong’o alilovaa kwenye tuzo za 2015 Oscars ameamua kulirudisha baada ya kugundua kuwa ni feki na halina thamani iliyotajwa.

Gauni hilo la Calvin Klein lililotengenezwa maalum kwaajili ya Lupita, lilimvutia mwizi huyo kulinyemelea na kuliiba baada ya kudaiwa kuwa na thamani ya $150,000 (zaidi ya shilingi milioni 274).

Mwizi huyo aliwapigia simu mtandao wa TMZ na kuwaelekeza alipoliacha begi lenye gauni hilo, na TMZ walitoa taarifa polisi ambao walilifatilia na kulikuta limerudishwa hotelini lilipoibiwa lakini likiwa limewekwa bafuni chini ya sinki.

Mtu huyo aliiambia TMZ kuwa aliliiba gauni hilo kwenye chumba cha Lupita baada ya kukuta mlango ukiwa wazi, na kubandua vigolori viwili na kuvipeleka kwa wataalam wambao walimwambia ni za bandia.

Mwizi huyo aliongeza kuwa aliamua kurudisha gauni hilo na kuwapigia simu TMZ ili kuumbua uongo wa mastaa wa Hollywood, na ulimwengu ujue kuwa gauni hilo halina thamani iliyotajwa.

No comments:

Post a Comment