TTCL

EQUITY

Monday, March 16, 2015

MAMLAKA YA MAWASILIANO TCRA YAKANUSHA KUWA NA MPANGO WA KFUNGIA MITANDAO YA KIJAMII

Baada ya Gazeti Moja Kubwa Kuandika kuwa TCRA ipo Mbioni kufunga Mitandao ya Kijamii inayotumika Vibaya ..TCRA wameibuka na Kusema :

'TCRA haina mpango huo na haikusudii kufanya hivyo na haina Mamlaka ya kufungia mtandao uliosajiliwa nje ya Tanzania.

Tumejikita zaidi kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi mazuri ya mawasiliano. Wanaotumia mitandao vibaya ni wachache kuliko wanaotumia vizuri

Habari hii sio kweli hakuna wakati wowote ambapo yeyote katika mkutano huo alizungumzia kufunga mitandao ya kijamii. Kwa mtu anayefahamu teknolojia anaelewa madhara na hasara ya kufanya hivyo.

Waandishi wa habari wanaaswa kuwa makini wanapoandika habari kuepusha kutoa habari ambazo sio sahihi na zinazoweza kuleta mtafaruku kwa jamii'

No comments:

Post a Comment