Jeshi la wananchi wa Tanzania limewaondoa hofu watanzania kuhusu tishio la matukio ya kigaidi na kuongeza kuwa jeshi hilo liko imara kukabiliana na hatari yeyote huku mahusiano baina ya Tanzania na Malawi yakielezwa kuwa imara na ya kindugu kufuatia ziara ya kikazi ya mkuu wa majeshi ya Malawi kuzuru hapa nchini kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya majeshi ya Tanzania na Malawi.
Mkuu wa majeshi ya Malawi jenerali Ignacio Maulana mara baada ya kuwasili katika viwanja vya makao makuu ya jeshi yaliyoko Upanga jijini Dar es Salaam amepata heshima ya kukagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake na mwenyeji wake jeneral Davis Mwamunyange na kisha kupata fursa ya kufanya mazungumzo ya faragha.
Mara baada ya mazungumzo ya faragha baina ya wakuu hao wa majeshi ya Tanzania na Malawi wamejitokeza mbele ya waandishi wa habari ambapo mkuu wa majeshi ya Tanzania jenerali Davis Mwamunyange amezungumzia pia suala la matishio ya kigaidi hapa nchini na kuwaondoa hofu watanzania kwakusema jeshi hilo liko imara.
Kwa pamoja wakizungumzia mahususiano baina ya nchi hizo wakuu hao wa majeshi wamesema uhusiano ni imara ambapo viongozi wakuu wa kitaifa pamoja na wale wa kijeshi wanapata fursa ya kutembeleana huku mkuu wa majeshi ya Malawi akisema kuwa mahusiano baina ya nchi hizo hayawezi kuchukuliwa kimzaha kwa kuwa ni ya kihistoria.
Mara baada ya mazungumzo hayo wakuu hao wa majeshi wameelekea Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuonana na rai
No comments:
Post a Comment