Hatuhitaji mikataba feki itakayo wanufaisha viongozi wenye tamaa na wasio kua na huruma dhidi ya watanzania. Zilitafunwa pesa za #EPA,#RICHMOND na za akaunti ya #TEGETA_ESCROW mmeona haitoshi mmeanza kuingilia mfuko wa jamii VICOBA kupitia FOCUS VICOBA kwa kutaka kutengeneza mikataba ya ushirika na bank kuu ya Tanzania (BOT) kwa maslahi yenu binafsi kitu ambacho sio sahihi.
Kumbukeni kua VICOBA ni Taasisi ya utoaji mikopo nafuu kwa kila mtanzania na imeundwa Taasisi hii kwa sharti la kuwapatia mikopo watanzania wote kwa kulenga kuwapatia mitaji ya fedha na kukidhi mahitaji yao na kuwaendeleza kiuchumi tena kwa masharti rahisi ili kila mtanzania wa hali ya chini aweze kunufaika na mfuko ulioundwa wa FOCUS VICOBA.
Uadilifu mbovu wa viongozi wenye tamaa mmepanga njama za kutaka kuingia ushirika na Taasisi hii kwa madai kua yakutaka kuboresha huduma za utoaji mikopo na kusaidia watanzania wakati inafahamika wazi kua bank ya BOT haina mamlaka ya utoaji mikopo kwa watanzania kama ilivyo asasi zingine za kifedha, pia hakuna uwiano kati ya VICOBA na BOT kulingana na umiliki tofauti nikiwa na maana kwamba VICOBA ni mfuko wa jamii ni asasi ya mtu binafsi inayoendesha shughuli za utoaji mikopo kwa watanzania na BOT ni Taasisi ya kifedha inayoendeshwa na Serikali inashughulika zaidi na uzalishaji wa fedha halali za malipo kwa matumizi ya watanzania.
Itawezekana vipi Taasisi hizi mbili kua washirika na kuendelea kutoa misaada ya fedha kwa watanzania kupitia utoaji mikopo wakati zinafanya kazi tofauti kulingana na Leseni zao zilivyo sajiliwa na hata mikataba ya utendaji kazi?
Hivyo zitakapo ingia ushirika itabidi zivunje mikataba ya usajili hasa hasa BOT na ikivunja mkataba itabidi itumike mikataba feki ili mradi lengo lao litimie kufanya kazi pamoja kama watadanganya watanzania katika mikataba watashindwaje kudhulumu haki ya wanyonge wasiokua na kitu wanao tegemea mikopo kupitia VICOBA??
Inafahamika wazi kua BOT ndio iliisaidia Taasisi ya VICOBA kupata wataalam wa IT kutengeneza Tovuti maalum ya mfuko wa FOCUS VICOBA ambayo ni www.vicobatanzania.wapka.mobi tovuti ambayo kila mtanzania anauwezo wa kuingia na kuomba mkopo kupitia ONLINE na kupatiwa mkopo. Tunashukuru watanzania wengi wamekua wakitembelea hii tovuti www.vicobatanzania.wapka.mobi na kujiunga na kupatiwa mikopo.
Ila kusaidia kwenu ukamilishaji wa hii tovuti isiwe chanzo cha kutaka kuhamisha umiliki wa vicoba kuvuruga uongozi wa Taasisi na kupoteza haki ya wajasiriamali ili mpeane mikopo wenyewe kwa wenyewe.
Hatuhitaji kusikia kashfa nyingine za mikataba feki ya kuwaumiza watanzania.
No comments:
Post a Comment