TTCL

EQUITY

Saturday, November 8, 2014

Ulipata alichokizungumza kapteni Komba kuhusu Mzee Warioba na Kinana? ninacho hapa

image-06-11-14-04-17-10Mbunge wa Mbinga Magharibi John Komba Novemba 6 2014 alikua miongoni mwa waliosimama na kuwasha kipaza sauti kwa ajili ya kuzungumza kwenye kikao cha Bunge ambapo aliyazungumza haya…
1- Kuhusu kauli ya Mbunge Peter Msigwa juu ya Katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana; “..kwa kuanza kwanza ni.. sikupenda sana kwa hotuba aliyoitoa mwenzetu Msigwa jana kuhusu katibu wetu mkuu Kinana wa CCM.. nataka nimuhakikishie Msigwa.. kati ya makatibu wakuu tuliowapata katika Chama cha Mapinduzi..waliokifanyia vizuri chama chetu cha mapinduzi… Kinana ni miongoni mwao na ndio tishio la upinzani kwa sasa hivi.. Kwa hiyo kumuingiza Kinana pale kumletea maneno ambayo hajayasema.. ni kiwewe tuu cha buree cha bure.. Kinana yupo pale kuwaondoeni nyie mnaosema mtachukua nchi…”—Komba
Komba
2- Kuhusu alichofanyiwa Jaji Warioba; “.. Pili nitoe pole kwa mzee Warioba.. juzi yale yaliyompata pale siyo jambo jema.. na yeye anasema kwamba hayajawahi kuona tangu uhuru.. lakini angesikia ushauri wangu wakati ule wa Bunge la Katiba haya yasingetokea.. akae tuu pembeni .. aache mjadala wao uendelee kama kawaida na utaratibu uende kama kawaida yeye alimaliza kazi yake.. wengine wafanye kazi yao na katiba hii mwisho ipatikane nzuri.. ukiingilia ingilia hayo ndiyo yatakayokupata.. mzee pumzika tuu…”– Komba

No comments:

Post a Comment