TTCL

EQUITY

Monday, November 17, 2014

TEKNOLOJIA YAKUA, MANYOYA YA KUKU YATUMIKA KUTENGENEZA VYANDARUA VYA KUZUIA MBU

nett 

Umewahi kufikiria manyoya ya kuku yanaweza kutumika kuwa kinga ya kuzuia mbu?hii ni kweli baada ya wataalamu wa mambo ya afya kudhibitisha hilo na kusisitiza ina uwezo huo kama ilivyo kwa vyandarua vinavyotengenezwa viwandani.

Wanasayansi kutoka Taasisi ya Afya Ifakara ‘IHI’ wamegundua mradi wa kutengeneza vyandarua kwa kutumia manyoya ya kuku yaliyorundikwa nyumbani na majalalani ikiwa ni moja ya jitihada za kuendeleza vita dhidi ya ugonjwa wa malaria hasa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Kwa mujibu wa taarifa ya utafiti wa kila mwezi iliyotolewa na Taasisi hiyo kwenye Gazeti la NIPASHE,manyayo hayo yatakua yanakusanywa kutoka maeneo ya masoko na kwenye makazi ya watu.

Kukamilika kwa mradi huo wa ubunifu utakua ni sehemu ya kupunguza takataka zinazotokana na mlundikano wa manyoya yaliyozagaa maeneo mbalimbali na kukabiliana na ugonjwa wa malaria ambao ni hatari kwa afya za wengi.

Wataalam wa afya wanaeleza kuwa vyandarua vimethibitishwa kuwa na uwezo wa kumkinga mtu dhidi ya maambukizi ya malaria lakini familia nyingi bado hazina uwezo wa kuzinunua.

henssss

Kwa mujibu wa utafiti huo,manyoya yanayofaa kwa ajili ya kutengeneza vyandarua hivyo vya kujikinga dhidi ya mbu,kwa lugha ya kisayansi inaitwa ‘Keran Fibers’ ambayo ni nyepesi,imara na havipitishi joto kwa haraka na hivyo kuweza kudumu kwa muda mrefu.

Mbali na kusaidia kukabiliana na malaria,mradi huo pia utaleta matokeo chanya katika utunzaji na kuibua fursa nyingi za kibiashara.

Utafiti huo ulifanywa na DK.Samson Kiware na Isaac Lyatuu kutoka Taasisi hiyo kwa ufadhili wa Grand Challenge Canada.

No comments:

Post a Comment