MWANANCHI
Mjane wa Baba wa Taifa,Maria Nyerere amesema Wabunge wanatakiwa kuijadili kwa kina ripoti ya Mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali kuhusu akaunti ya Escrow kwa kuwa kuficha mambo kutaendelea kuzidisha matatizo nchini.
Alisema njia pekee ya kumaliza suala hilo linalotarajiwa kuwasilishwa bungeni leo,ni kwa wabunge kujadili taarifa hiyo na kuchukua hatua zinazostahili.
Mama Nyerere alisema suala hilo linagusa maslahi ya umma hasa katika kipindi hiki ambacho wengi wanakosa huduma muhimu kutokana na uhaba wa fedha unaoikabili nchi.
“Wanaposikia ripoti za ukaguzi wanafichwafichwa wakati ndugu zao wanakufa kwa kukosa dawa,ni lazima watakua na hasira na baadaye kusababisha machafuko”alisema Mama Maria.
MWANANCHI
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Mkoani Kigoma,Felix Mkosamali amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Kibondo akikabiliwa na shtka la kumzuia karani mwandikishaji kufanya kazi yake.
Mwendesha mashtaka wa Polisi,Peter Makalla alidai mahakamani hapo kuwa mbunge huyo alitenda kosa hilo juzi baada ya kufika kwenye kituo cha kupigia kura na kumzuia karani kuendelea kuandikisha wakazi kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali ya mitaa.
Makalla alidai kitendo cha kumzuia karani huyo kuendelea kufanya kazi yake ni kinyume na ukiukwaji wa sheria ya uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Pia alidai kitendo cha kuwazuia wakazi hao kupiga kura ni kuwanyika haki zao za msingi,kwani walipozuiwa waliendelea kudai kutaka kujiandikisha lakini mshtakiwa hakusikiliza kilio chao.
MWANANCHI
Siku moja baada ya Mbunge wa Musoma vijijini Nimrodi Mkono kusema amelishwa sumu akiwa London Uingereza,Mbunge wa Chadema Halima Mdee amemtaka kusema ukweli na si kulihadaa Taifa kwa uongo.
Mkono alisema leng la kulishwa sumu ni kutaka kuharibu figo zake ndani ya saa72 lakini kitendo hicho kilichoshindikana.
Mdee aliyekua na Mkono katika ziara hiyo nchini Uingereza alisema hakuna ukweli wowote kuhusu yeye kutaka kulishwa sumu,nilikua naye kule na mazingira ya kuanza kuumwa hadi kupona kwake ni utata mtupu….awaeleze Watanzania anaumwa nini na si kusingizia alilishwa sumu,”alisema.
‘Kama anataka kutumia kivuli cha Escrow,arudi bungeni tuweze kujadili na tuimalize ili asiseme kuwa sijui wanataka kumuua ni uongo.
MWANANCHI
Pamoja na maneno mengi yaliyosemwa,shutuma lukuki zilizotolewa na mbinu za kila aina kutaka kuzuia mjadala wa ripoti ya uchaguzi wa kashfa ya IPTL leo ndio hukumu yake.
Katika hukumu hiyo ukweli utadhihirika kuhusu nani mkweli na nani mwongo wakati kamati ya bunge itakapowasilisha Bungeni maoni yake kuhusu ripoti ya kuchotwa kwa zaidi ya bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Mapema jana Spika wa Bunge Anne Makinda alisema ripoti hiyo itajadiliwa na hakuna wa kuizuia licha ya kuwepo kesi iliyofunguliwa mahakamani kuzuia mjadala wa ripoti hiyo.
Katika mlolongo wa vitisho David Kafulila jana alipokea ujumbe wa simu ukisema “Nadhani umeamua kifo kwa kutafuta sifa za kijinga,nakuhurumia sana maana hujui unapambana na nani,huu ni ujumbe wa mwisho kama huamini utaamini kaburi
JamboLEO
Bunduki zaidi ya 200 zimekamatwa Wilayani Kiteto,Mkoani Manyara ili kubaini kama ili kubaini kama zilitumika kufanya uhalifu au mauaji ya watu saba yaliyotokea Wilayani humo hivi karibuni.
Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara Deosdedit Nsimeck alisema hatua hiyo inasaidia kubaini silaha zinazofanya matukio ya kihalifu katika maeneo mbalimbali Wilayani Kiteto.
“Silaha hizo kutoka kwa wananchi,tumeamua kuzikusanya kutoka kwa wananchi zikiwemo zile zinazomilikiwa kihalali na isivyo halali ili kudhibiti vitendo vya kiuhalifu vinavyoendelea kujitokeza ikiwemo mauaji ya mara kwa mara.
MTANZANIA
Aliyekua Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amewataka viongozi wa Serikali kutomtukana na kumkejeli ili kujitafutia ushindi.
November2 Warioba alifanyiwa vurugu na watu wanaodhaniwa kuwa ni wanachama wa CCM katika mdahalo wa katiba ulioandaliwa na Taasis ya mwalimu Nyerere kwenye hotel ya Blue Pearl Jijini Dar es salaam.
Warioba alisema viongozi wamekua wakimtukana na kumkejeli kutokana na msimamo wake na kazi aliyoifanya katka tume ya mabadiliko ya Katiba.
“Napata tabu kuona viongozi wanatafuta ushindi kwa kunitukana,eti Wariobana wenzake wamemsaliti mwalimu Nyerere,hivi angekuwepo angeyakataa haya ya maadili?mwalimu kabla ya kufa alisema tuweke ukomo wa uraisakijua kuwa utaanzia kwake,marais wengine wanataka aendelee,”alisema Warioba.
NIPASHE
Tanzania ina uwezo wa kuzalisha tani zaidi ya milioni6 za saruji ikilinganishwa na mahitaji ya tani milioni3.2 kwa mwaka.
Waziri wa Viwanda na biashara Janet Mbene alisema kutokana na Tanzania kuzalisha kiwango kikubwa cha saruji,ina zaidi ya tani milioni 2.8 ya kuuza nje ya nchi.
Kuhusu viwanga Mbene alisema Tanzania ina viwanda vitano vilivyo katika kiwango kizuri vya uzalishaji wa saruji nchi nzima.
NIPASHE
Kasheshe iliibuka katika kituo cha uandikishaji wa wakazi katika kata ya Msogola Jijini Dar baada ya makarani kuandikisha majina kwenye kituo bubu na shule ya msingi Mbondole.
Tukio hilo lilitokea baada ya wanachama wa CUF tawi laMbondole kubaini mbinu hiyo kuwa inaweza kutumika kuandikisha majina ya watu ambao si wakazi wa eneo husika.
Wanachama hao wa CUF walikua wamejiandaa wakiongozwa na mgombea wao wa nafasi ya uenyekiti lakini wanachama hao, hivyo kwa pamoja wanachama wa CUF na CCM walikubaliana kuyachoma moto na kuanza upya zoezi hilo
No comments:
Post a Comment