TTCL

EQUITY

Saturday, November 29, 2014

YANAYOJIRI BUNGENI - (HALIMA MDEE NA MNYIKA WAFUNGUKA YA KWAO JUU YA ESCROW)


Kama ilikupita hii tazama yaliyojiri usiku wa kuamkia Nov 29 2014 kabla ya kusonga mbele...

Na baada ya jana bunge kuahirishwa usiku, Leo saa tatu limerejea tena na aliekalia kiti ni mama Anna Makinda na ambapo aliahirisha bunge mpaka saa tano asubuhi kupisha vikao vya vyama(caucus) kuketi.


MAJADILIANO YANAENDELEA

Lukuvi: Kama ulivyotoa taarifa ya kuahirisha bunge asubuhi nia yako ilikuwa tupate maazimio yatakayo tuunganisha wabunge ili tuwe na maazimio yenye maridhiano yanayokubalika ndani na nje. Wabunge tumetumia fursa ya kukaa kwenye vyama, CCM tumekaa kwa na tumefanya baadhi ya marekebisho ili tutoke na maazimio, tunaomba tuendelee na majadiliano na naomba utuongezee saa moja.

Mnyika: Waziri amesema mashauriano (consultation) zinazoendelea ni za CCM hatuwezi kutoka kama bunge moja kama mashauriano ya CCM yanaenda kuchakachua mapendekezo ya kamati hivyo yasiwe mapendekezo ya wabunge, naomba muongozo hii habari ya kuweka maazimio ya chama kwa kutumia wingi wao kwenye bunge.

Lukuvi: Naomba tushaurine kwa pamoja nje ya bunge na niko sawa na Mnyika. Naomba uturuhusu tupate saa moja tushauriane kama bunge nje ili tupate muafaka.

Spika: Kimataifa ndivyo tunavyofanya, Naagiza viongozi wa upinzani na wenzao wakae pamoja maana hatutafika na anapendekeza mpaka saa kumi.

Zitto: Saa kumi mbali sana, serikali imeomba saa moja hivyo napendekeza masaa mawili tu, saa kumi ni mbali sana. Baada ya masaa mawili turudi hapa tuendelee na kazi za bunge.

Mbatia: Nakubaliana na hoja ya waziri, watu wakishauriana vizuri itaondoa mivutano na kuondoa mambo ya uchama na tukija hapa muda utakuwa mfupi wa kumalizia. Napendekeza saa nane ili iwe masaa matatu kwani saa kumi itatoa mda mchache.

Sendeka: Nakubaliana na mapendekezo lazima watayoyaleta tukubali hapana maana wanaweza kushindwana. Tuwashauri waende na naunga mkono hoja ya saa kumi lakini mimi ningependelea saa tisa.

Wenje: Napendekeza mashauriano, kamati iundwe wakakubaliane na turudi saa kumi ili vikao vya vyama(causus) vipewe muhtasari(briefed) walichoafikiana

Makinda: Nataka turudi saa kumi, wale viongozi wetu wakakae pamoja.

Silinde: Naungana na suala la saa kumi, lakini kwa sababu kumekuwa na tuhuma nyingi, napendekeza wote waliotumiwa kwenye ripoti wasihudhurie kwenye mashauriano.

Makinda: Na mimi pia nilikua nafikiria hivyo pia Zitto achukue watu wake wachache wahudhurie na naahirisha bunge mpaka saa kumi.


Bunge limekutana tena sasa na msemaji wa kwanza aliyekaribishwa ni @jjmnyika

@jjmnyika : Utata uliokuwepo juu ya kifo cha Mh. William Mgimwa aliyekuwa Waziri wa fedha, wengine wakausisha kifo kile na ulaji wa fedha hizi za Escrow

Mnyika: Muhongo lazima awajibike kwa kujizuru na lazima awajibike kwa wananchi
Mnyika: Linapokuja suala la uwajibikaji kwa Mawaziri wa kawaida linaonekana sawa ila inapokuwa Waziri Mkuu mnamkingia kifua
Mnyika: Kama mtakumbatia hili suala tutachukua hatua za kupiga kura juu ya kukosa imani na Waziri Mkuu:
@halimamdee : Mwanasheria Mkuu unatakiwa utupishe uende Tarime ukapumzike
@halimamdee : Tukirogwa tukianza kudai kodi manaake ni kwamba serikali tumehararisha wizi huu
@halimamdee : Mahakama kuu ya Tanzania haikuwa na mamlaka yoyote kushughulikia fedha za ‪#‎TegetaEscrow‬

No comments:

Post a Comment