Wakati kukiwa na maneno mengi juu ya madai ya kuvunjika kwa ndoa yake na prizenta maarufu Bongo wa Redio E-FM, Gardner G Habash ‘Kepteini’, supastaa wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo a.k.a Jide au Jaydee amefunguka kuwa naye si mkamilifu kwani siyo Yesu wala Bikira Maria.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, wikiendi iliyopita Jide aliamua kuvunja ukimya kufuatia maswali ya mashabiki wake lukuki waliotaka afunguke kinachoendelea katika maisha yake.
Judith Wambura Mbibo a.k.a Jide au Jaydee.
“Watu wanategemea niwe kama Yesu au Bikira Maria? Siwezi, mimi ni mwanadamu tu. Hakuna aliye mkamilifu. Niacheni niishi maisha yangu bila stresi. Mwingine yeyote pia aishi maisha yake. Kila mmoja anatakiwa awe huru,” aliandika Jide.
No comments:
Post a Comment