TTCL

EQUITY

Thursday, November 20, 2014

MIONGOZO YA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA



1. Fuata maagizo kwa uangalifu.
2. Usibadili kiasi cha dawa bila kumuuliza daktari.
3. Usiache kutumia dawa ulizoandikiwa bila kuagizwa na daktari.
4. Usipondeponde au kuvunja tembe ikiwa hujaagizwa kufanya hivyo.
5. Tambua madhara ambayo dawa hizo zinaweza kukusababishia unapoendesha gari au unapofanya utendaji mwingine.
6. Chunguza madhara ya kuchanganya dawa hiyo na alkoholi au dawa nyingine, iwe umeandikiwa na daktari au umeinunua bila maagizo ya daktari.
7. Ikiwa umewahi kutumia dawa vibaya au vitu vingine vinavyolewesha, mwambie daktari.
8. Usitumie dawa alizoandikiwa mtu mwingine, na usiwape watu wengine dawa ulizoandikiwa.*

No comments:

Post a Comment