TTCL

EQUITY

Tuesday, November 4, 2014

Mariah Carey hutumia shilingi milioni 142 kujiandaa kwaajili ya kupiga picha!


Kwa mujibu wa kesi iliyofunguliwa na mpiga picha mmoja dhidi yake, Mariah hutumia kiasi kikubwa cha fedha kujiandaa kwaajili ya photoshoot. Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa muimbaji huyo mwenye miaka 45 anahitaji kupambwa kwa gharama ya $85,000 (zaidi ya shilingi milioni 142) kabla hajaanza kupigwa picha.

Nyaraka hizo zinadai kuwa Mariah anahitaji huduma hiyo kutoka kwa stylist maarufu anayegharimu $65,391. Kisha kuna mtu anayemtengeneza nywele, $9,600 na make-up artist, $7,200. Kutengeneza kucha zake pia hugharimu $2,400.

Mpiga picha huyo aliamua kushtaki baada ya kujiandaa kwa photoshoot kwaajili ya kava la album yake ambayo ilisitishwa bila sababu. Anataka alipwe $150,000 za ada ya huduma hiyo.
 

No comments:

Post a Comment