Story za maajabu ya ulimwengu zinaendelea kukaa kwenye headlines kila siku, na inaponifikia cha kwanza ninachokifanya ni kukufikishia mapema iwezekanavyo ili na wewe usipitwe.
Ya leo inaweza kuwa moja kati ya zilizowahi kukushangaza zaidi, inahusu mwanamke Janina Kolkiewicz raia wa Poland, mwenye umri wa miaka 91 ambaye amekaa kwa muda saa 11 katika chumba cha kuhifadhia maiti huku mwili wake ukiwa ndani ya jokofu baada ya kuthibitishwa na daktari wa familia yake kwamba amefariki, muda mfupi baadaye wahudumu wa mochwari waligundua kwamba ni mzima baada ya kuhisi anatikisika ndani ya mfuko alimowekwa.
Baada ya kurudi nyumbani kwake akitokea mochwari, alilalamika kuhisi baridi kali na kupatiwa bakuli la supu ya moto na mkate.
Daktari aliyethibitisha mauti ya mtu huyo anasema hata yeye anashangazwa na tukio hilo kwani vipimo vyote vilionyesha kuwa mapigo ya moyo yalisimama na hakuwa hai.
Taarifa za kuwa hai mwanamke huyo zilimshtua kila mtu kwenye familia yake na kujikuta ikibatilisha hati ya kifo iliyotolewa kwa ajili ya mazishi yake ambayo yalipangwa kufanyika siku mbili baadaye..
No comments:
Post a Comment