TTCL

EQUITY

Wednesday, October 29, 2014

MIMBA za utotoni ni tatizo nchini kwetu


MIMBA za utotoni ni tatizo nchini kwetu. Kwa mujibu wa Takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, wasichana 8000 kila mwaka huacha shule kutokana na ujauzito. Katiyao3,000 ni wanafunzi wa shule za msingi.
Kila siku, wanawake 24 hufariki dunia kutokana na mimba au wakati wa kujifungua. Wanawake watano mpaka sita wanaofariki kati ya hao ni watoto wadogo.
Ni ukweli usiopingika kuwa, watoto hao hufariki dunia kwa kuwa miiliyaohaijakomaa vya kutosha kwa ajili ya kujifungua. Pia wanapopata mimba wasizozitarajia huzitoa kwa njia zisizo salama.
Naibu mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Watoto (UNICEF), Mohamed Safieldin anasema mbali na athari hizo, pia virusi vya ukimwi (VVU), vinavyosambaa kwa kasi kwa wasichana hao.Tanzaniakuna watoto yatima milioni 1.3 walioathirika kwa ukimwi.
Katika miaka ya karibuni, tatizo la mimba za utotoni mkoani Mtwara limeanza kupungua kutokana na jitihada zinazofanywa na wanaharakati mbalimbali.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Umoja, mkoani Mtwara, ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa Mapambano dhidi ya Ukimwi Shuleni (PASHA), Beatrice Masanja, anasema mradi huo umekuwa na manufaa kwa wanafunzi kwani umewasaidia kujitambua.
Kwa mujibu wa mwalimu Masanja, Pasha imesaidia shule kadhaa katika utambuzi wa athari za mimba utotoni. “Shule nyingi ambazo mradi huu upo, mimba za utotoni zimepungua pamoja na maambukizi ya virusi vya ukimwi,” anasema na kuongeza kuwa, kupitia mradi huo vijana wanatakiwa kujitambua, hivyo inakuwa rahisi kujua jambo hili ni sahihi ama laa, pamoja na kutambua vishawishi, ngono na mimba za utotoni.
Anasema, vijana wanao uelewa kuhusu miiliyao, waliowazidi umri na pia jinsi ya kujizuia. Anaeleza changamoto waliyonayo ni kwamba wameshindwa kupanuka zaidi na kufikia shule zote katika mkoa huo. Kwani mpaka hivi sasa wapo kwenye shule 72 za msingi kati ya zaidi 500 na sekondari 20 kati ya 133.
Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Sabin Sirima, anaeleza kuwa tatizo la watoto kupata mimba linatokana na utamaduni wa eneohilo.
“Ukishakuwa na utamaduni ambao vipaumbele vyake si elimu inaleta shida. Hapa kuna masuala ya Jando na unyago, ngoma kuchezwa, watoto pia wanafundishwa masuala ya ndoa hivyo inajengeka akilini mwao kuwa wana uwezo wa kupata watoto,” anasema Sirima.
Mkurugenzi huyo anaonya kuwa, masuala hayo ya utamaduni si mambo ya kuyaingilia kwa haraka, ni mambo ya kwenda nayo taratibu.
“Sisi tuliwaambia ninyi watu wa Mtwara kila siku mnalalamika kuwa nafasi za juu za uongozi zinashikiliwa na wageni, lakinikamamngechukua nafasi zenu na kusoma, nyie ndio mngechukua nyadhifa hizi.
“Hapa hali ipo tofauti kidogo na maeneo mengine, mtoto anaweza kuambiwa asifaulu ili aolewe na imeshawahi kutokea,” anasema.
Sirima anasema, kwa upande mwingine wazazi nao wanachangia watoto wao kukatiza masomo na hatimaye kupata ujauzito.
“Kamaserikali tumekuwa tukijitahidi wale wanaofaulu kuwapeleka sekondari lakini wanatoroka…mwaka huu watoto 47 wamefaulu lakini hawajaenda shule, wanatoroka wanaolewa na kupata mimba,” anasema mkurugenzi huyo.
Kwa mujibu wa Sirima, hivi sasa katika mkoa huo, kesi za mimba zimekuwa zikifuatiliwa na vyombo vya dola, pamoja na kutangaza kwa bidii sheria ya kujamiiana na ile ianyokataza ubakaji.
Pia elimu imekuwa ikitolewa kwa bidii na wanawake kutoka Umoja wa wanawake wa mkoa huo (UWT) na maofisa maendeleo ya jamii. Viongozi hawa kwa kushirikiana wamekuwa wakizungumza na wanafunzi wa kike mashuleni.
Hali hiyo imesaidia kwa kiasi kikubwa kubadili mwelekeo wa wanafunzi kuwa wakipata sekondari wanapomaliza msingi, wanakwenda. Kutokana na hali hiyo, hivi sasa wasichana wengi wanamaliza darasa la saba tofauti na ilivyokuwa awali.
Kwa upande wake Ofisa Elimu wa Wilaya, Eddy Mbele, anasema kuwa, mila na desturi kwa kiasi kikubwa imechangia mimba za utotoni katika umri mdogo.
“Vile vile masuala ya jando, unyago na kipato kidogo kwa wenyeji wa mkoa huo, navyo vimechangia hali hiyo,” anasema.
Naye Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto katika Mkoa wa Mtwara, Vivian Kilimba anasema wamekuwa wakitoa elimu mashuleni inayolenga afya kwa wanafunzi. Pia kuhusu masuala ya uzazi, wamekuwa wakizungumzia magonjwa ya ngono pamoja na ukimwi.
“Tumekuwa tukitoa vipeperushi, elimu kwa walimu ili nao waweze kutoa huduma rafiki kwa vijana. Sera ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, inaruhusu kutoa elimu ya uzazi kwa vijana wenye umri wa miaka 15 na kuendelea,” anasema mratibu huyo.
Naye hakusita kueleza kuwa, katika mkoa huo, tatizo la mimba za utotoni ni kubwasanakwa wasichana walio chini ya miaka 18.
“Tunachokiona hapa inakuwa ni ufahari kuwa aliyemaliza darasa la saba ana uwezo wa kuwa na familia yake, hivyo anaamua kuolewa,” anasema.
Hakusita kueleza kuwa, watoto hao wanapata matatizo kiafya wakati wa kujifungua kwa kuwa miiliyaohaina uwezo wa kupokea hali hiyo, suala la lishe nalo ni tatizo kwa kuwa familia nyingi zinaishi maisha duni.
Anaeleza matatizo mengine yanayoweza kuwapata watoto hao ni uchungu wa muda mrefu, au uzazi pingamizi kwani hushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mtwara Vijijini, Dk. Magreth Mwakyusa, anasema kuwa, mtoto anapopata mimba katika umri mdogo anakuwa hana uamuzi wa afya yake, katika kujieleza anapopatwa na uchungu au hali anayoihisi.
Hawana uwezo wa kujikimu, pia tegemezi kwa wazazi wake, anaongeza mzigo mwingine kwa familia. Ujauzito katika umri mdogo matatizo yanakuwa ni makubwa hivyo huhitaji uangalizi wa karibu katika hospitali kubwa.
Mganga huyo anaeleza kuwa, si jambo la kushangaza katika mkoa huo, kuwaona wasichana wenye umri wa miaka 19 au 23 wakiwa wamejifungua mara nne, na asilimia kubwa ya wasichana hao hupata fistula.
Akielezea takwimu za miaka mitano iliyopita za wasichana wenye umri mdogo kupata mimba alitaja idadi ya wasichana ilifikia 24,236.
Anasema, mwaka 2005 wasichana wenye umri mdogo waliopata mimba walikuwa 3871; mwaka 2006 walikuwa 4886; mwaka 2007 walikuwa 4616; mwaka 2008 walikuwa 4697 na mwaka jana walikuwa 6166.
Anasema, mwaka jana idadi iliongezeka kwa sababu kabla ya hapo, wengi wao walikuwa ni waogo wa kuhudhuria klinic, lakini mwaka jana wengi wao walihudhuria.
Vile vile alizitaja takwimu za wanafunzi walioacha mimba kutokana na ujauzito kuwa mwaka 2005 waliacha wanafunzi 421; mwaka 2006 waliacha 297; mwaka 2007 waliacha 231 wakati mwaka 2008 walioacha walikuwa 197.
Anasema, takwimu zinapungua mwaka hadi mwaka kutokana na elimu inayoendelea kutolewa, pamoja na walimu kusimamia kwa bidii sualahilolimewafanya wanafunzi wenyewe kuimarika na kujua umuhimu wa elimu, sekondari za kata nazo zimesaidiasana.
Msichana Edna Alawi wa kijiji cha Namikupa Tandahimba ni miongoni mwa wasichana ambao wamekatisha masomo baada ya kupata mimba za utotoni, hapa akimnyosha mtoto wake wa miezi 8 na nyuma yake kuna mtoto wake wa mwaka mmoja na miezi sita.

Kulea kusaidiana, kijana huyu alikutwa katika hospitali ya Wilaya ya Tandahimba akimsindikiza mkewe kuwatibia watoto wao mapacha.

Mganga mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Tandahimba Bw.Idd Msonde akiongea na waandishi wa habari hawako pichani juu ya mimba za utotoni na ugonjwa wa fistula.


Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya kutwa Namikupa wkiingia ndani ya nyumba waliyopangakamabweni la wavulana kijijini hapo.

Wanafunzi wa Shule ya sekondari Namikupa wakichota maji kisimani umbali wa kilometa tatu kutoka kijijini wanapoishi na kusoma.

No comments:

Post a Comment