TTCL

EQUITY

Thursday, October 2, 2014

UANDISHI WA HABARI, NA UTANGAZAJI


Chunguza picha za udanganyifu na hila

Yeyote yule anayekuletea picha aghalabu huziambatanisha na maelezo fulani. Jiepushe kuzikubali picha zisizo na maelezo yoyote. Mtu anayekuletea picha na akaandika “hizi ni picha nzuri” aghalabu huwa amezinyakua kutoka kwenye intaneti

Namna ya kuchunguza picha za udanganyifu na hila zilizoletwa na mtumizi wa mtandao
1. Mtumiaji Baruapepe
Mtumie baruapepe yule aliyekuandikia baruapepe.  Ipate nambari yake ya simu na, ikiwezekana, mpigie simu uzungumze naye.
  • Anaweza kuielezea picha aliyoleta? (Jibu lake linalingana na ripoti za mashirika ya habari zinavyosema kuhusu yaliyotokea?)
  • Muulize alikuwa wapi na yuko wapi sasa? (Akisema kwamba yuko kwenye mkahawa wa intaneti basi utafute kwenye mtandao wa Google).
  • Muulize nani alizipiga picha.
  • Muulize picha zilipigwa kwa kutumia chombo gani.
2. Zifanyie uchunguzi picha hizo kwa kulinganisha na zile za mashirika ya habari.
Je, hizi picha ni nzuri sana kuweza kupigwa na mtu wa kawaida? Ikiwa una shaka basi fanya uchunguzi kwa kuangalia picha za mashirika ya habari kwenye mitandao ya Elvis, Yahoo or Google — unaweza ukazikuta hapo.  TinEye ni mtandao mpya unaoweza kukufanyia kazi hiyo!
3. Inamkinika amezipiga picha ZOTE?
Mpiga picha huyu anakwenda kwingi. Ikiwa atakuletea picha nyingi, basi jiulize kweli mtu huyu amefika kote huko na kuzipiga picha zote hizo?
4. PowerPoint? Tahadhari
Ikiwa picha ulizoletewa umeletewa kama maonyesho ya slaidi ya ‘PowePoint’, au ikiwa umeletewa zaidi ya mara moja, basi kuwa na shaka. Pingine mtu amezipata kutoka vyanzo mbalimbali na akazikusanya pamoja.
5. Hakuna maandishi? Tahadhari.
Yeyote yule anayekuletea picha aghalabu huziambatanisha na maelezo fulani.  Jiepushe kuzikubali picha zisizo na maelezo yoyote. Mtu anayekuletea picha na akaandika “hizi ni picha nzuri” aghalabu huwa amezinyakua kutoka kwenye intaneti.
Na kuna ishara zinazoweza kukuhakikishia ikiwa hizo picha ni za kweli na si za udanganyifu:
6. Zikague pixel (elementi za picha)
Ukubwa wa picha: angalia vipimo vya picha kwa pixel.  Picha asili zinazopigwa kwa kamera daima huwa za ukubwa wa takriban 2,000 x 1,200 na zaidi.  Picha yoyote iliyo ndogo kuliko vipimo hivyo basi imepunguzwa vipimo.
Angalia vipimo vya nambari za witiri — yumkini picha zenye vipimo hivyo zikawa zimechukuliwa kutoka picha za mashirika ya habari.  Kwa mfano, aghalabu picha za habari za Yahoo zina vipimo vya upana wa 380 na urefu wa 345.
Unaweza pia ukapima maelezo ya EXIF (ya faili za kubadilisha picha), yanayoweza kukwambia picha zilipigwa lini na yakakupa dalili nyingine.
7. Haimkini kuwa nzuri hivi?
Wakati mwingine unaweza kusema haimkiniki picha zikawa nzuri hivi lakini sio zile zilizo kwenye mitandao ya mashirika ya habari.  Huenda zikawa zimetengenezwa kwa kutumia programu kama za Photoshop.  Muombe mtu mwenye Photoshop kwenye kompyuta yake aitoe picha hiyo na halafu aivute kwa karibu. Angalia wapi viwango vya rangi vinapokutanika na angalia iwapo yale matabaka yenye sehemu nyingi yameingiliwa. Huenda ukapata taabu kugundua kwa sababu mbano wa jpeg (wa kupunguza ukubwa wa picha) utaiathiri picha.
Bila ya shaka, huna haja ya kufanya ukaguzi wote huu kila wakati, kwani unahitaji kuzirusha hewani picha.  Lakini ikiwa una shaka, basi kagua!
Ni muhimu kwamba ufanye kazi zako kwa haraka.  Aghalabu picha za watumizi wa mtandao na maelezo yao ndiyo mambo ya mwanzo unayoyapata kuhusu ripoti fulani na unataka kuzirusha kabla ya kupata mambo mingine. Huna muda mwingi. Ikiwa umezoea kufanya ukaguzi wa kuthibitisha kwamba picha na mingine uliyoletewa ni sahihi basi mchango wa mtumizi wa mtandao hurushwa hewani kwa haraka.
Kuthibitisha Baruapepe za watumizi wa mtandao
Baruapepe za udanganyifu na hali zinazusha matatizo.
Kuthibitisha baruapepe kama ni za kweli, unachukua nyingi ya hatua unazochukua kuthibitisha kama picha ni za kweli na sahihi.  Na hatua hizohizo unawachukulia wale wenye kupiga simu BBC wakidai kwamba wameshuhudia tukio fulani la habari.
1. Ijibu Baruapepe anayokuletea mtu
Ikiwa unamtaka aliyekuletea baruapepe au taarifa ya maandishi azungumze hewani, au ukiwa unataka kumtumia kama sehemu ya ripoti unayoandika kwenye mtandao, basi ni MUHIMU kuwapigia simu kuthibitisha kama kweli walilishuhudia HASA tukio waliolieleza kwenye baruapepe yao ya awali.
2. Muombe picha
Muombe akuletee picha yake.  Akikubali kukuletea picha, basi inamkinika sana kwamba ni yeye aliyekuandikia baruapepe.  Haya bila ya shaka hayawezekani palepale habari inapotokea.
3. Lisake jina lake kwenye intaneti
Lisake jina lake kwenye mtandao wa Google (au mtandao wowote mwingine wa kusaka mambo), na hasa angalia ikiwa ana ajenda fulani.  Huenda akawa ni mmoja wa wafanyao kampeni kuhusu jambo fulani — angalia mafungu ya maneno yanayotumiwa sana katika baruapepe kama hizo.
4. Angalia alama za eneo lake
Angalia alama ya nambari ya simu ya eneo analopigia simu na anuwani ya baruapepe yake. Zipo kweli?
5. Chunguza maelezo mingine
Mshikilie akupe maelezo zaidi ikiwa utataka kuyatumia maelezo aliyokuletea katika baruapepe yake.

No comments:

Post a Comment