Vidokezo vya matangazo ya redio
Kwa hivyo unahitaji kuwaeleza
jambo fulani kuhusu yaliyomo katika kipindi – unahitaji kuwapa habari
za kutosha zitakazowatia mshawasha wa kusikiliza, lakini kuna hatari
kwamba ukiwaeleza mengi kupita kiasi huenda hawatataka kusikiliza zaidi
kwani tayari wamekwisha pata habari za kutosha.
Jinsi ya kutayarisha vidokezo vya matangazo ya redio: na Jonathan Stoneman
Kwa kawaida taarifa za habari na vipindi vingi vya matukio ya kisasa huanza kwa vidokezo au muhtasari wa dakika moja. Muhtasari huo huangazia yaliyomo katika kipindi chako, sawa na vioo vya maduka vinavyoonyesha yaliyomo.
Kwa mintarafu wa mfano huo, hungependa watu wafurahie tu wanachoona kwa nje; ungependa waingie dukani na kununua bidhaa fulani.
Kwa hivyo unahitaji kuwaeleza jambo fulani kuhusu yaliyomo katika kipindi – unahitaji kuwapa habari za kutosha zitakazowatia mshawasha wa kusikiliza. Lakini kuna hatari kwamba ukiwaeleza mengi kupita kiasi huenda hawatataka kusikiliza zaidi kwani tayari wamekwisha pata habari za kutosha.
(Pia, hatari nyingine ni kwamba ukiwapa wasikilizaji taarifa tatu au nne kuu basi wataacha kusikiliza wakishasikia habari ulizozitangaza katika muhtasari. Hivyo basi, unahitaji kutia ndani angalau taarifa moja nyingine itakayokuja baadaye katika kipindi chako.) Unataka waketi na kusikiliza, kwa hiyo hutawaeleza habari zote – watie mshawasha wa kujua mengi zaidi.
Kwa kawaida taswira mbalimbali hutumiwa katika vidokezo. Jaribu kutumia sehemu zilizomo katika kipindi hicho – mapambo ya sauti, manukuu, na visehemu vya mahojiano. Jambo lolote linalowafanya watu watake kusikiliza na kujua mengi zaidi; kidokezo chochote kitakachoamsha hamu, au pengine kinachozusha swali.
Vidokezo vya matangazo ya redio MMX 2
Mtangazaji anayeuliza maswali katika kidokezo anaweza kutimiza mengi sana – k.m. 'Huenda ungepitia hapo miaka 100 iliyopita katika gari lako lenye kukokotwa na farasi, lakini vipi leo, unaweza kupitia hapo katika gari lako?' (unapozungumzia hali ya Blackwall Tunnel huko London) …
(Maswali yana faida - lakini je, utafurahia kusikiliza kipindi ambacho huanza kwa maswali tu kila siku?)
Bado itakubidi ufuate Kanuni za Uhariri za BBC - usahihi, haki, kutopendelea …
Utayatimiza yote hayo kwa dakika moja tu!
Unahitaji kufikiri. Hakikisha umefikiria mapema vidokezo utakavyotumia (andika vidokezo vyako mara uamuapo yaliyomo katika kipindi), kwa sababu itafaa mtangazaji wako avirekodi kabla havijachelewa mno.
No comments:
Post a Comment