TTCL

EQUITY

Thursday, October 2, 2014

JIFUNZE UANDISHI WA HABARI, NA UTANGAZAJI HAPA

Ili usikike vizuri kabisa

Huna haja ya kupiga kelele na kuzungumza kwa sauti kubwa kwa sababu huhutubii umati wa watu. Wala usisikike ukitoa sauti kama ya mtu mwenye kuwatangazia watu wazima malai tamu; hivyo ndivyo utavyosikika ikiwa utanong’ona karibu sana na mikrofoni.

Baadhi ya mbinu za kutumia vyema mikrofoni na kuhakikisha unatumia vizuri mikrofoni na unahakikisha sauti yako ni halisi na ya kuburudisha.
Mwalimu wa sauti Elspeth Morrison ana ushauri wa namna ya kukufanya uzungumze kwa kuvutia kwenye mikrifoni.
Kwanza anashauri  usiiweke mikrofoni karibu sana na mdomo wako kama vile unavyowaona waimbaji wanavyofanya.  Kuzungumza na kuimba si sawa, ni mambo tofauti.
Badala yake, anakushauri uifanye mikrofoni kama sikio la mwanadamu na iwe mbali nawe kama sikio la mtu mwengine lilivyo mbali nawe.
Pia ni muhimu nguvu ya sauti iwe sawa.
Huna haja ya kupiga kelele na kuzungumza kwa sauti kubwa kwa sababu huhutubii umati wa watu.  Wala usisikike ukitoa sauti kama ya mtu mwenye kuwatangazia watu wazima malai tamu; hivyo ndivyo utavyosikika ikiwa utanong’ona karibu sana na mikrofoni.
Kumbuka kuvuta pumzi
Ikiwa huvuti pumzi kikawaida basi utasikika kama una wasiwasi.
Elspeth anaeleza kwamba kwa kusahau kuvuta pumzi unaweza ukakabwa na ukaanza kusitasita isivyo kawaida –  hakuna mtu atayetaka kukusikia hivyo.
Kwa hivyo, ili kukusaidia uweze kuvuta pumzi mahali ndipo hakikisha kwamba umeweka alama zilizo wazi katika taarifa yako.  Tumia alama ya kituo kwa kuvuta sana pumzi na kijikoma kidogo cha kuvutia pumzi kwa haraka ili umalize kusoma sentensi. 
Kuitunza Sauti Yako
Itunze sauti yako na hakikisha kwamba imechangamka kabla ya kuanza kutangaza.
Mwalimu wa sauti Elspeth Morrison anaeleza kwamba kwa mwandishi mtangazaji sauti yako ni nyenzo muhimu ya kazi yako.
Kwa hivyo inahitaji kuangaliwa.
Nini kizuri? Maji ndio rafiki yako mkubwa.  Daima hakikisha kwamba umekunywa maji vya kutosha siku nzima unapokuwa unatangaza au unarikodi vipindi.
Na nini kibaya?
Elspeth anashauri tuwe waangalifu wa vitu kama sigara, kahawa, vyakula fulani na baadhi ya madawa — vitu ambavyo vinaweza kuikausha sauti yako au kuiathiri vibaya.
Kila mtu ana vitu vinavyomfaa yeye kuifanya sauti yake iwe ya kuvutia; kwa hivyo ushauri mzuri ni kuangalia nini kinachokufaa na nini cha kukiepuka.
Kuchangamka
Sauti yako inaonyesha jinsi mwili wako unavyohisi.  Mbinu ya kukufanya usikike kama umechangamka nyakati za usiku sana au alfajiri sana ni kujifanya kama uko macho kabisa hata ikiwa huhisi hivyo.
Kuna mbinu mbili unazoweza kuzitumia ili sauti yako isikike kama uko macho kabisa kwa muda mfupi.
Elspeth anashauri  uangalie namna unavyokaa unapokuwa unarikodi kipindi  —ukijibwaga kitini sauti yako inaweza ikawa chapwa isiyokolea. Baadhi ya watu huona afadhali wasimame.  Na kama katika maisha yako ya kawaida una desturi ya kuzungumza na huku unatumia ishara ya mkono basi jaribu kufanya hivyo pia unapotangaza — ama sivyo hutosikika kama mtu anayezungumza kama kawaida yako.

No comments:

Post a Comment