Mshtuko! Siku chache baada ya kujiengua kwenye nafasi
ya uenyekiti katika Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’ anadaiwa kufutwa uanachama wa klabu hiyo.
Aliyekuwa mwenyekiti katika Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Chanzo cha ndani ya klabu hiyo kimepenyeza madai kuwa, wameamua
kumvua uanachama Steve kwani wanaona ni ‘kirusi’ ndani ya klabu kutokana
na mwenendo wake.
“Steve amekuwa akiwashawishi baadhi ya memba wajiunge na upande wake,
tofauti na umoja wa Bongo Movie Unity, viongozi wameamua kumfuta kabisa
uanachama,” kilisema chanzo na kuongeza:
“Amewatangazia wenzake vibaya juzikati alivyokwenda Dodoma kwenye
sherehe za kukabidhiwa kwa Rasimu ya Katiba Iliyopendekezwa kwa
kuwaambia viongozi wa serikali kwamba wasanii ambao hawakwenda mjini
humo ni Ukawa wakati si kweli.”
Katibu wa Bongo Movie Unity,William Mtitu akiwa ndani ya Ofisi za Global.
Baada ya chanzo chetu kujiridhisha na data hizo za ndani, mwanahabari
wetu alimtafuta Steve Nyerere ili kujua anazungumziaje juu ya ishu hiyo
ya kuenguliwa klabuni na mtazamo kuhusu suala hilo, alipopatikana
alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi ni mwanachana wa Bongo Muvi kama nimefutwa sijui lakini ni
mwanachama. Kuhusu kuwasemea nilipokuwa Dodoma, ningewasemea mimi kama
nani? Sina cheo cha kuwasemea wenzangu.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na tafrani kubwa Bongo Muvi huku madai mengi yakielekezwa kwa Steve.
No comments:
Post a Comment