TTCL

EQUITY

Monday, October 20, 2014

SAKATA LA MABOMU ARUSHA MTUHUMIWA AUAWA NA POLISI

Mtuhumiwa wa Milipuko ya mabomu jijini Arusha Auawa kwa kupigwa risasa na Jeshi la Polisi wakati akijaribu Kuwakimbia.

Polisi mkoani Arusha wamuua kwa risasi mtuhumiwa Namba Moja wa milipuko ya mabomu katika mikusanyiko jijini humo na umwagiaji watu tindikali baada ya kujaribu kutoroka akiwa njiani kwenda kuonesha bomu alilokuwa amelificha maeneo ya Kondoa mkoani Dodoma.

Jeshi  la  polisi  mkoani  arusha  limemuua  kwa  kumpiga  risasi  mtuhumiwa  namba  moja  wa  wa milipuko  ya  mabomu  katika  mikusanyiko  na  kuwamwagia   viongozi  wa  dini  tindikali  baada   ya  kujaribu  kutoroka  akiwa  chini   ya  ulinzi  akiwa  njiani  kwenda  kuonyesha  bomu  alilokuwa amelificha  maeneo  ya  kondoa  mkoani   dodoma.
Akitoa  taarifa  za  kifo  cha  mtuhumiwa  huyo   kamanda  wa  polisi  wa  mkoa  wa  arusha  Lebaratus   Sabas  amesema  marehemu   yahaya  hassan omari  hela  maarufu  kwa  jina  la  (SENSEI) ambaye  alikuwa  anatafutwa  kwa  muda  mrefu.  
Mtuhumiwa  huyo   alikamatwa  wiki mbili zilizopita  mkoani  morogroro  na  kupelekwa  arusha  na  bado  alikuwa  anaendelea  kuhojiwa.
Kwa  mujibu  wa  kamandaa  Sabas  mtuhumiwa  marehemu  yahaya  alishakiri  kuwa  yeye  ndiye  alikuwa  msimamizi  mkuu   wa   matukio  yote   ya  milipuko   ya  mabomu na  ya  kumwagia  viongozi  wa  dini  tindikali  yaliyowahi  kutokea  mkoani  arusha  na  maeneo  mengine.
Aidha  kamanda   Sabas  amefaanua  kuwa  baada  ya  marehemu  mtuhumiwa  kukiri  tuhuma  hizo  alikuwa  bado  anaendelea  kutoa  ushirikiano   kwa  kuanza  kuonyesha  vitendea  kazi   yakiwemo    mabomu  ambayo  alidaiwa  kuyaficha  kondoa  mkoani  Dodoma.
Amesema   wakati   anasafirishwa   walipofika  eneo  la  kisongo   katika  barabara kuu inayoenda  dodoma  majira ya  usiku   alifanya  jaribio  la  kutaka  kutoroka  na  ndipo  akapigwa  risasi   iliyomjeruhi  mguu  na  kiuno   na  akafariki  wakati  anapelekwa hosipitali.

No comments:

Post a Comment