Pamechimbika! Staa wa sinema za Kibongo, Aisha Bui
amezua timbwili la kufa mtu katika ofisi za kusambaza filamu za Yuneda
zilizopo Mbagala jijini Dar baada ya wasambazi hao kushindwa kumlipa kwa
wakati.
Staa wa sinema za Kibongo, Aisha Bui akiwaka kwa mmoja wa wahusika wa ofisi za kusambaza filamu za Yuneda, Mbagala.
Mtiti huo ulioshuhudiwa na wanahabari wetu ulijiri wikiendi
iliyopita, maeneo hayo ya Mbagala ambapo Aisha aliongozana na shemeji
yake katika ofisi hizo na kuibua tafrani kubwa iliyokusanya kadamnasi na
kufunga mtaa kwa muda.
Aisha Bui mara baada ya kuvunja kioo cha mlango.
Kwa mujibu wa Aisha, amekuwa akitimba kwenye ofisi hizo mara kwa mara
akiomba alipwe chake lakini amekuwa akipigwa kalenda tangu Aprili,
mwaka huu. Aisha alilifungukia Ijumaa Wikienda kwamba, kuna siku
mkurugenzi wa kampuni hiyo aitwaye Ngeze alimwita ofisini kwake ili
kumlipa lakini alipofika alimpa kiasi cha shilingi milioni mbili na
nusu, jambo ambalo lilikuwa kinyume na makubaliano.
Aisha Bui akiwa na jiwe lililotumika kuvunjia mlango wa kioo wa ofisi hizo.
“Filamu yenyewe nimeigiza kabla sijajifungua hadi mtoto wangu sasa
ana miezi sita. Kama mtu ndiyo unategemea fedha za filamu yako ndiyo
uendeshee maisha, halafu mtu halipi, sasa utaishije?
Staa huyo alisema alikuwa akimpigia simu mara kwa mara mwisho mkurugenzi
huyo aliamua ‘kum-block’ kwenye simu hivyo akawa amekosa mawasiliano
naye.
Wananchi wakishuhudia varangati lililoanzishwa na Aisha Bui.
Aisha alipofika ofisini hapo alishikwa na ghadhabu baada mhasibu wa
kampuni hiyo kumwambia hakuwa na namba ya bosi wake wakati alijua
akifika tu angepewa fedha hizo hivyo akashikana naye mashati na kuanza
kuzipiga ambapo Aisha alisukumwa akadondoka pwaa!
Kitendo cha kusukumwa, kilimpandisha hasira Aisha na kuamua kuchukua
jiwe ambalo lilishindwa kufungua mlango hivyo alichukua nondo na kuvunja
mlango huo ambapo wafanyakazi walijifungia kwa ndani ili kumzuia
asiingie ndani.
Aisha Bui akiondoka eneo la tukio.
Wanahabari wetu walipomfuata Ngeze kujua kulikoni kumtia mbaroni
Aisha alisema alivamiwa na staa huyo na mabaunsa ambao walivunja ofisi
pamoja na kushukua ‘laptop’ na fedha.
Hadi gazeti hili linaondoka eneo hilo, Aisha na shemeji yake walikuwa
bado wameshikiliwa na Polisi wa Kituo cha Maturubai, Mbagala.
No comments:
Post a Comment