Kufuatia taarifa zilizozagaa mjini morogoro na kuripotiwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mbunge wa jimbo la morogoro kusini, Dk Lucy Nkya na mwanaye Jonas Nkya ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa kupitia vijana, kurushiana risasi kwenye ofisi yao binafsi ya faraja trust fund, watu hao wawili wamekanusha madai hayo na kudai yameleta athari kubwa katika familia yao.
Awali taarifa zilizojitokeza na baadaye kurushwa kwenye mitandao
mbalimbali ya kijamii, ilikuwa ni mama huyo aliyewahi kuwa naibu waziri
wa afya, na mwanaye ambaye ni mjumbe wa NEC akiwakilisha vijana,
kurushiana risasi kwa kugombea nyumba iliyotaka kuuzwa jijini Dar es
salaam, hali iliyofanya ITV kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa
morogoro Leonard Paulo ambaye kwa njia ya simu amekiri tukio la mlio wa
risasi kujitokeza katika ofisi za faraja, lakini mazingira yake hawezi
kuzungumzia hadi arudi ofisini, kwavile alikuwa safarini.
Hata hivyo Jonas Nkya alipopatikana amekanusha madai hayo na kwamba
kilichojitokeza ni kuanguka kwa bastola yake iliyokuwa kiunoni, baada
ya kwenda ofisi za faraja kubadilisha gari kwaajili ya kwenda shamba,
ambapo ilijifyetua risasi mbili na kutoa mlio uliosababisha baadhi ya
watu kusogea eneo hilo na kwamba kama kungekuwa na ugomvi wa kifamilia,
ungefanyika nyumbani kwao ambapo yupo kwa sasa, akimsaidia mama yake
kumuuguza baba yake Prof Nkya,ambaye amepooza, madai ambayo yameungwa
mkono na mama yake mzazi ambaye naye amehojiwa katika ofisi za faraja,
baada ya kukutwa akiendelea na majukumu yake.
No comments:
Post a Comment