TTCL

EQUITY

Tuesday, October 7, 2014

KATIBA MPYA YAMWONDOSHA MWANASHERIA ZANZIBAR

Ccm inatia aibu. Ina maana kura zilizopigwa Dodoma hazikua za maamuzi ya mtu binafsi? Zilikua kura za maelekezo? Hatuna bunge kama hali ni hii.
 Julius S. Mtatiro's photo.
Julius S. Mtatiro added 2 new photos.
MWANASHERIA MKUU ALIYEIKATAA RASIMU YA KATIBA, AMEFUKUZWA KAZI!!
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, amemuondoa Mwanasheria Mkuu wa SMZ, Mhe. OTHMAN MASOUD OTHMAN (Kushoto) na amemteua Mhe. SAID HASSAN SAID (Kulia) kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na Uteuzi huo umeanza leo 7, Oktoba 2014, kabla ya uteuzi huo Mhe, Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa SMZ.
Mabadiliko haya ni kwa mujibu wa uwezo ambao Rais wa Zanzibar amepewa chini ya Kifungu 55(1) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984.
MY TAKE………
Narudia tena maneno yangu ya tarehe ya Tarehe 01 Oktoba 2014, kwamba “……Huyu hatafuti kazi, kazi zinamtafuta yeye……”
Na leo naongeza maneno mengine kuwa “….dunia inahitaji binadamu shupavu kama huyu, wasiouza taaluma, ujuzi, ubobezi na weledi wao kwa vipande vya fedha na madaraka….”
MUNGU AKUPE NGUVU NA AFYA OTHMAN!!!
J. Mtatiro,
DSM.

No comments:

Post a Comment