
Uhusiano
na mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2013, Latifa Mohamed wenye miezi
tisa sasa, ndio uhusiano mrefu zaidi aliowahi kuwa nao Ben Pol tangu awe
staa ameongea na chanzo makini juu ya mahusiano yake yaliyopita
yalishindwa kudumu kwakuwa wasichana wengi walikuwa na matarajio makubwa
kutoka kwake kwakuwa yeye ni msanii. Sasa hivi tuna miezi tisa, nadhani
ndio the longest relationship, amesema Ben kuhusu uhusiano na Latifa.
“Unajua nimekutana na watu wa aina tofauti.
Nimekutana
na watu ambao labda wanakuwa na expectations kubwa zaidi kuhusu mtu
fulani, kwahiyo akiingia kwenye maisha yako labda kuna vitu ambavyo yeye
tayari alishapicture,labda Ben Pol tutakuwa tunakula bata every
weekend, tunakula bata milioni, tunaenda huku kule everyday.
Kwahiyo mtu anaweza akaja kwenye maisha yako akakuta sio mtu wa hivyo, ni staa ndio lakini you dont go to clubs
mara kwa mara, you dont do this, you dont do that kama mastaa wengine. Kwahiyo mtu anakuwa disappointed anatoka kwenye maisha yako. Ndio hicho ambacho nimeexperience zaidi kwenye mahusiano yangu yaliyopita.
mara kwa mara, you dont do this, you dont do that kama mastaa wengine. Kwahiyo mtu anakuwa disappointed anatoka kwenye maisha yako. Ndio hicho ambacho nimeexperience zaidi kwenye mahusiano yangu yaliyopita.
Kwahiyo
ukipata mtu ambaye akakuelewa hivyo, inatia moyo kidogo. Ben Pol
amesema hata hivyo uhusiano wake na Latifa haujawa rasmi kabisa kwakuwa
bado hajaenda kujitambulisha kwao. Lakini at least naweza kusema nina
hatua moja katika tano au katika tatu.”