Taasisi ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi AMUA ikiwa ni programu mpya chini ya shirika la PSI leo wamekutana na wakazi wa Jijini Arusha na kutoa elimu na burudani kwa njia ya sanaa kwa kuwatumia vijana wenye vipaji mbalimbali kutoka Arusha, na kuhamasisha maelfu kupima afya zao.
Aidha wakazi wa arusha walitoa ushiriki wao kwakushiriki vilivyo kwakuonesha burudani mbalimbali, kadhalika msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo flava nchini, Chid Benzi naye alitoa burudani ya ainayake, nakuweza kukonga nyoyo za mashabiki na watu wote walio hudhuria katika tamasha hilo.
Taasisi hiyo inayoratibiwa na Mh. Esteria Kisoka imeonesha kupokelewa kwa furaha, huku vijana wakijitokeza kwa wingi na kushiriki elimu juu ya maambukizi ya virusi vya ukimwi, uaminifu, maamuzi sahihi kuhusu mahusiano na kujitambua. kulingana na kauli mbiu iliyokuwa ikisema AMUA wakati ni sasa, maelfu ya watu walijitokeza na kuamua kujua afya zao.
tamasha hili lilianza Dar es salaam, na sasa wakafikia Arusha ambapo kwa siku moja walihusisha mikoa miwili Arusha na Mwanza ambapo huko walikuwepo washiriki na mabalozi wa AMUA walio husika kutoa elimu. kulikuwepo burudani za hapa napale, kukimbia na maguni, kukimbia na ndimu, kukimbia na vijiti, kuvuta kamba, maigizo, free style na kucheza.
hizi ni baadhi ya picha za matukio yaliyojiri Arusha.
 |
Msanii Chid Benzi |
 |
Wakazi wa jiji la Arusha wakitazama burudani ya tamasha la AMUA |
 |
Washiriki wa shindano la AMUA wakiwa katika mchezo wa kuvuta kamba |
 |
Washiriki wa shindano la AMUA wakiwa stejini wakitoa burudani kwa watazamaji |
 |
Wakazi wa Arusha wakitoa burudani ya kichekesho katika tamasha la AMUA |
 |
Hapa wakionesha igizo la michepuko, elimu ya uzazi na majukumu ya wazazi kwa watoto |
 |
Crew ya viongozi na wasanii wa AMUA |
 |
Wasanii wa ngoma za asili wakitoa burudani na ujumbe wa mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi |
No comments:
Post a Comment