millardayo.com imekua na mfululizo wa kukuletea picha za nyumba za kisasa zilivyojengwa kwenye nchi za wenzetu ili angalau kama unapenda mabadiliko wa muonekano wa kisasa upate chochote cha kuiga kutoka kwao.
Asilimia kubwa za hizi nyumba madirisha na milango havijazingatia hatari ya wezi kutokana na mazingira yao ila kwa Tanzania ni ngumu kufanya hivi japo kuna baadhi ya nyumba nimeshawahi kwenda nikakutana na kitu kama hiki lakini zote zina uzio mkubwa kuzizingira.
Pamoja na kwamba kuna uwezekano wa kushindwa kujenga nyumba kama hii Tanzania naamini unaweza kupata chochote kitu mfano mimi hapa leo nimependa mpangilio wa taa za nje na ndani, rangi ya ukuta, muonekano wa nje kwenye picha ya kwanza na hizi picha nyingine zinazofata hapa chini.
Wakati mwingine vitu vidogo kama hii garden huwa vinanifanya nidate, ni garden ndogo lakini simple na nzuri
No comments:
Post a Comment