
HUKU
wadau mbalimbali wa Habari wakiendelea kulaani vikali kitendo cha Jeshi
la polisi kuwapiga wanahabari wakati wakiwa kazini katika tukio
lilitokea Mwishoni mwa wiki iliyopita Makao makuu ya Jeshi la polisi
nchini wakati Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Freeman Mbowe akijisalimisha polisi, Katika hali ya kushangaza Serikali imesema haina taarifa juu ya kupigwa kwa mwandishi yoyote wa habari.
Kauli
hiyo ya Kushangaza imetolewa leo jijini Dar Es Salaam na Mkurugenzi wa
Idara ya Habari Maelezo, Asah Mwambene alipokuwa anatembelea miradi ya
maendeleo ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mbagala Jijini Dar Es
Salaam.
Tanesco imetimiza miaka 50 toka ianze kutoa huduma ya usambazaji nishati kwa wananchi nchini kote.
Tanesco imetimiza miaka 50 toka ianze kutoa huduma ya usambazaji nishati kwa wananchi nchini kote.
Mmoja
wa waandishi wa habari aliyekuwepo katika ziara hiyo (toka gazeti la
mwananchi) alitaka kupata kauli kutoa kwa Mkurugenzi huyo kuhusiana na
tukio lililofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya wanahabari waliokuwepo
kazini wakati Mbowe akifika Polisi.
Mwambene
ambaye pia ni Msemaji wa Serikali alisema, hana taarifa za kupigwa kwa
waandishi wa habari bali katika tukio hilo lililohusisha wanachama wa
Chadema kukusanyika makao makuu ya jeshi hilo wakati kiongozi wao
akijisalimisha.
“Serikali haina taarifa za kupigwa kwa waandishi, nakuomba tuzungumeze vitu vingine ”Alijibu Mwambene.
Hata hivyo baadhi ya watu walisikika wakinong'ona wakisema; “tumemsikia
mwandishi mmoja akilalamika sana kwenye vyombo vya Habari, ni Josephat
Isango wa gazeti la Tanzania Daima ambaye anaeleweka kabisa kwamba ni
mwanachama wa chadema."
Mnong'onezaji huyo alisikika akisema Isango aliwahi kugombania Ubunge kupitia chama hicho.
Mnong'onezaji huyo alisikika akisema Isango aliwahi kugombania Ubunge kupitia chama hicho.
Kauli
hiyo ya Mwambene inatafsiriwa tofauti na wadau wa Masuala ya Habari
kwani kuzungumza huku kunazidisha maswali mengi kutokana na Idara ya
habari maelezo ndio inayowasimamia Waandishi pamoja na Magazeti.
Kwa
Upande wake, Josephati Isango amenukuliwa akithibitisha kuwa na nia ya
kumburuza mahakamani CP Chagonja, polisi watatu waliompiga pamoja na
Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
“Nawasiliana
na wanasheria wangu watatu jinsi ya kwenda mahakamani kuwashitaki
polisi watatu, Cp Chagonja na waziri mkuu ambaye mnakumbuka alishawhi
kutoa maagizo ya kupiga watu ovyo yanayotekelezwa na Polisi
hivisasa,”alisema Isango.
No comments:
Post a Comment